MASELE ACHANGISHA SH. MILIONI 25 KUNUNUA VYOMBO VYA KISASA VYA MUZIKI KANISA LA MORAVIAN SHINYANGA MJINI


Mhe. Stephen Masele akiendesha harambee
Stephen Masele (katikati akiwa ndani ya kanisa la Moravian Shinyanga Mjini
Aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini na Makamu wa kwanza wa Rais wa Bunge la Afrika (PAP) Stephen Masele amechangisha shilingi Milioni 25 Kanisa la Moravian Mjini shinyanga katika harambee ya kuchangia ununuzi wa vyombo vya Muziki vya kisasa vya kanisa hilo.


Harambee hiyo imefanyika leo Jumapili Julai 31,2022 katika Kanisa la Moravian Mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na mamia ya waumini wa kanisa hilo.

Akizungumza wakati wa harambee hiyo Mchungaji kiongozi wa Kanisa hilo Jonas Ludonya amelezea furaha yake kwa kufanikiwa kumpata mbunge mstaafu Stephen Masele.


"Kwa kweli tumefurahi sana kuwa naye hapa leo kama unavyoona waumini wakimfurahia mhe Masele, ni mtu wa watu na mnyenyekevu mwenye upendo wa kweli kwa wana Shinyanga, unaona jinsi anavyoshangiliwa na waumini”, amesema.


Mheshimiwa Masele yupo Shinyanga kwa mapumziko na ameshiriki shughuli mbalimbali za kijamii ikiwemo kuhudhuria shughuli ya upadrisho ya Padre Emmanuel Gimbuya wa Buhangija Shinyanga mjini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments