ANAYETAKA KUNUNUA MTANDAO WA TWITTER AANZA KUZINGUA


Billionea Elon Musk (Anayetaka kuachana na mpango wa kuinunua twitter)

Elon Musk anataka kuacha azma yake ya kununua mtandao wa kijamii wa Twitter kwa dola 44 (£36bn), akidai kuwa kumekuwa na uvunjaji wa mara nyingi wa makubaliano.


Tangazo hilo ni mabadiliko ya hivi karibuni katika sakata inayoendeelea baada ya mtu huyu tajiri zaidi duniani kuamua kununua Twitter mwezi Aprili.


Bw Musk amesema ameamua kujiondoa kwasababu Twitter ilishindwa kutoa taarifa za kutosha kuhusu idadi ya akaunti gushi na ambazo hazitumiwi.


Twitter inasema inapanga kuchukua hatua ya kisheria kutekeleza makubaliano.


"Bodi ya Twitter Board imejitolea kuzuwia uhamishaji wa fedha kuhusu bei na masharti yaliyofikiwa kati yake na Bw Musk,"Mwenyekiti wa Twitter Bret Taylor aliandika kwenye ujumbe wake wa Twitter, hatua inayoashiria uwezekano wa makabiliano ya muda mrefu ya kisheria baina ya pande hizo mbili.


Makubaliano ya makubwa ya awali yalijumuisha dola bilioni 1 (£830m) bila kuvunjwa.


Mzozo kuhusu akaunti gushi


Mwezi Mei, Bw Musk alisema mkataba ulikuwa "umezuiwa kwa muda" kwasababu alikuwa anasubiri data kuhusu akaunti feki na zisizotumiwa za Twitter.


Mfanyabiashara huyo bilionea alikuwa ameomba ushahidi wa kuthibitisha maelezo ya kampuni kwamba akaunti gushi na zile zisizotumiwa ni sawa na 5% ya watumiaji wa mtandao huo kwa ujumla.


Katika barua iliyowasilishwa na taasisi za usalama za Marekani na tume ya ubadilishaji wa pesa, wakili wa Bw Musk alisema kuwa Twitter ilishindwa au ilikataa kutoa taarifa hizi.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments