KIPEPEO PAD YAGAWA TAULO ZA KIKE KWA MABINTI SHULE YA SEKONDARI NDALA SHINYANGA


Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndala taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. Katikati ni Mwalimu wa Afya Shule ya Sekondari Ndala Leticia Kisima.
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
 Kampuni ya Kipepeo Pad inayojihusisha na utengenezaji na usambazaji wa Taulo za kike zinazojulikana ‘Kipepeo Pad’ imetoa msaada wa taulo za kike kwa wanafunzi wa kike 286 wanaosoma katika shule ya Sekondari Ndala Manispaa ya Shinyanga.


Kampuni ya Kipepeo Pad ambayo Mkurugenzi wake ni Janeth Dutu imetoa na kugawa taulo hizo za kike leo Alhamisi Julai 28,2022 ambapo mgeni rasmi alikuwa Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban ‘Tausi Coffee’.


Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi taulo za kike, Zamda ameishukuru Kampuni ya Kipepeo Pad kwa kuwajali na kuwathamini wanafunzi wa kike katika shule hiyo akibainisha kuwa zitawasaidia mabinti hao kujiweka safi na kujiamini hivyo kufanya vizuri katika masomo yao.


Zamda amewasihi wanafunzi hao kuzingatia masomo yao na kuhakikisha wanaepuka vishawishi vinavyoweza kusababisha washindwe kumaliza shule ikiwemo mimba na ndoa za utotoni huku akiwashauri kutoa taarifa pindi wanapoona kuna vitendo vya ukatili wa kijinsia.


Kwa upande wake, Mkuu wa shule ya Sekondari Imani Chambulilo amesema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 515 kati yao wasichana ni 286 ambao wamepatiwa taulo laini zitakazosaidia kuwafanya mabinti wajiamini na kuwa na utulivu darasani hivyo kuinua taaluma shuleni hapo.


Naye Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndala, Lucas Magandula amemshukuru Mkurugenzi wa Kampuni ya Kipepeo Pad, Janeth Dutu kwa kuiona shule ya Sekondari Ndala na kuipatia taulo za kike hivyo kuwaomba wadau wengine kuendelea kujitokeza kuchangia sekta ya elimu na shughuli zingine za maendeleo.
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akimkabidhi Mwalimu wa Afya Shule ya Sekondari Ndala Leticia Kisima, taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, Imani Chambulilo, kushoto ni  Afisa Elimu kata ya Ndala, Alphonsina Senduye. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akimkabidhi Mwalimu wa Afya Shule ya Sekondari Ndala Leticia Kisima, taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. Kulia ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Ndala, Imani Chambulilo, kushoto ni  Afisa Elimu kata ya Ndala, Alphonsina Senduye.
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndala taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. Katikati ni Mwalimu wa Afya Shule ya Sekondari Ndala Leticia Kisima.
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akimkabidhi Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndala taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndala, Lucas Magandula akionesha taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Muonekano wa maboksi yaliyobeba taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Muonekano wa maboksi yaliyobeba taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndala wakionesha taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ndala wakionesha taulo za kike zilizotolewa na Kampuni ya Kipepeo Pad kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akiishukuru Kampuni ya Kipepeo Pad kutoa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban akizungumza na wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Wanafunzi wakimsikiliza Diwani wa Kata ya Ndala Manispaa ya Shinyanga Mhe. Zamda Shaban.
Mkuu wa shule ya Sekondari Ndala akiishukuru Kampuni ya Kipepeo Pad kutoa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
 Afisa Mtendaji wa Kata ya Ndala, Lucas Magandula akiishukuru Kampuni ya Kipepeo Pad kutoa taulo za kike kwa ajili ya wanafunzi wa kike wa Shule ya Sekondari Ndala. 
Sehemu ya Wanafunzi wa kike wa shule ya Sekondari Ndala.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post