PADRI AUAWA KWA KUPIGWA RISASI


Padri aliyetekwa asadikika kuuawa

PADRI mmoja wa Kanisa la Katoliki anayefahamika kwa jina la John Mark Cheitnum ambaye alitekwa nyara akiwa na wenzake wawili, ameuawa kwa kupigwa risasi katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria.

Taarifa zinaeleza kuwa mauaji hayo yametekelezwa na watu wenye silaha waliovamia jimbo hilo na kwamba mwili wa padri huyo umegundulika jana Jumanne.


Padri mwengine aliyekuwa ni miongoni mwa waliotekwa nyara, Donatus Cleopas aliachiwa huru jana huku ikiwa bado haijafahamika chanzo cha mauaji ya Padri Cheitnum.


Taarifa zinaeleza kwamba mapadri hao walitekwa nyara kwa kutumia mtutu wa bunduki siku ya Ijumaa walipokuwa katika makazi yao kwenye kijiji cha Yadin Garu nchini Nigeria.


Mwenyekiti wa shirikisho la Wakristo wa Nigeria katika Jimbo la Kaduna, Joseph Hayab amesema kwamba watekaji nyara walipokea pesa kwa ajili ya kuwaachia hao mapadri.

Padri John Mark Cheitnum ameuawa katika Jimbo la Kaduna nchini Nigeria

Mwenyekiti Hayab ameeleza kuwa watekaji nyara waliowaongoza watu walioleta pesa za kuwakomboa mapadri hadi mahali ambapo ulikuwepo mwili wa padri aliyeuawa.


Ripoti inaleza kwamba tangu Mei, mwaka huu takriban makumi wa mapadri wa Kikristo, wengi wao wakiwa ni Wakatoliki wametekwa na watu wenye silaha Nigeria kote.


Serikali ya Nigeria inapitia wakati mgumu kutokana na kushindwa kukabiliana na ukosefu mkubwa wa usalama licha ya kusambaza maelfu ya wanajeshi katika nchi hiyo ili kukabiliana na watekaji nyara.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post