Breaking : RAIS SAMIA ATEUA MKUU MPYA WA JESHI LA POLISI TANZANIA...IGP SIRRO AONDOLEWA.

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amempandisha cheo Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura na Kumteua kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP).


Kupita taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu Zuhura Yunus imeeleza kuwa Uteuzi huo umefanyika usiku wa kuamkia leo Jumatano Julai 20, 2022 ambapo kabla ya kuteuliwa alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (CDI).

Pia Rais Samia amemteua aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Simon Sirro kuwa Balozi wa Tanzania Nchini Zimbabwe.

Wakati huo huo amempadisha cheo Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) Ramadhan Hamis Kingai kuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya Jinai (CDI).

Uteuzi mwingine ni kama ifuatavyo:Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments