MTALII AFARIKI KWA KUKATWA NA BAWA LA HELIKOPTA AKISHUKA
Eneo la tukio alipofariki kijana mwenye umri wa miaka 21 mtalii kutoka nchini Uingereza

MTALII kijana raia wa Uingereza mwenye umri wa miaka 21 amefariki baada ya kukatwa na bawa la helikopta mbele ya ndugu yake wakati wakitua kutoka katika mji wa Athens wakitokea katika mji wa Mykonos nchini Ugiriki walikoenda kwa ajili ya Utalii.


Taarifa zinadai baada ya kushuka alitembea nyuma ya mkia wa Helikopta huku injini ikiwa inaendelea kufanya kazi ndipo alipocharangwa vipande vipande huku ndugu yake akishuhudia tukio zima.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 12:20 jioni ambapo mara moja gari la huduma kwa wagonjwa lilifika mara moja kwenye Helikopta ambayo ilikuwa ni usafiri binafsi wa familia hiyo ya kitajiri.

Kijana huyo alifariki kwa kucharangwa na bawa la Helikopta

Tayari Rubani wa Helikopta hiyo ameshatiwa mbaroni huku waongoza ndege wa zamu nao wakitiwa nguvuni pia kwa ajili ya kupisha uchunguzi wa tukio hilo.


Kwa mujibu wa taarifa ya awali ya Polisi ni kwamba propela huzunguka kwa muda wa dakika 2 ikiwa ni baada ya Helikopta kutua au kubonyeza kitufe cha kuzima ndani ya sekunde 50 mara baada ya Helkopita kutua.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

Post a Comment

Previous Post Next Post