BARRICK BULYANHULU NA NORTH MARA KIDEDEA TUZO ZA TANTRADE


Mwenyekiti wa Bodi wa STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, (wa pili kulia) na Mkurugenzi wa STAMICO, DKt. Venance Mwesse (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na Meneja Uhusiano na Masuala ya ndani wa Barrick ,Neema Ndossi na Mratibu wa Uhusiano na Masuala ya Ndani wa kampuni hiyo, Abella Mutiganzi , baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt. Philip Isdory Mpango, wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam iliyofanyika jana. Barrick ilishinda tuzo za kuongoza kuuza madini katika migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara na tuzo ya mwasilishaji bora wa michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).
Wafanyakazi wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Abella Mutiganzi (kulia) wakifurahia tuzo za ushindi baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt. Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Meneja Masoko na Uhusiano wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) , Geoffrey Meena (katikati) akiwa na Meneja Uhusiano wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Mratibu wa Uhusiano na Masuala ya Ndani, Abella Mutiganzi (kulia) baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt.Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi wa STAMICO, Meja Jenerali Mstaafu Michael. Isamuhyo,(katikati) akibadilishana mawazo na wafanyakazi wa Barrick, Neema Ndossi (kushoto) na Abella Mutiganzi (kulia) baada ya kampuni hiyo kukabidhiwa tuzo za ushindi za TANTRADE na Makamu wa Rais DKt. Philip Isdory Mpango, wakati wa kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.
Baadhi ya wafanyakazi kutoka makampuni yaliyoshinda tuzo wakiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais DK.Philip Isdory Mpango, na viongozi wengine wa Serikali wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.


***


Kampuni ya Barrick kupitia migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara imeshinda tuzo za Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambazo zilikabidhiwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Philip Mpango, wakati wa hafla ya kufunga maonesho ya 46 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaam.


Tuzo ambazo kampuni imejishindia ni kuongoza kuuza madini nje ya nchi (Export Minerals Award) kwa migodi yake ya Bulyanhulu na North Mara na tuzo ya mwasilishaji bora wa michango ya wafanyakazi kwenye Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) – (Best Employer compliance) kwa mgodi wa Bulyanhulu.
Barrick, imetambulika kama mchangiaji mkubwa wa mapato ya Serikali katika mwaka wa 2021 na hivyo kuthibitisha nafasi yake kama mchangiaji mkubwa katika ukuzaji wa uchumi wa kijamii Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments