KABAKA AKUTANA NA UWT SHINYANGA...ATAKA WANAWAKE KUCHANGAMKIA NAFASI ZA UONGOZI CHAGUZI ZINAZOENDELEA CCM

Mwenyekiti wa Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza kwenye mkutano na wanawake wa UWT mkoani Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka, amewaasa wanawake wa UWT hapa nchini, wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi ndani ya jumuiya na chama.

Amebainisha hayo leo Juni 28, 2022 mkoani Shinyanga, kwenye ziara yake ya kikazi, wakati akizungumza na Jumuiya ya Wanawake Tanzania (UWT) mkoani Shinyanga.

Amesema ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), hivi sasa kuna chaguzi za viongozi zinaendelea, na kuwasihi wanawake wajitokeze kwa wingi kugombea nafasi hizo.

"Nipo katika ziara ya kikazi, na kipindi hiki Chama chetu cha Mapinduzi (CCM) tupo kwenye uchaguzi wa ndani ya chama na katika Jumuiya zetu zote tatu, hivyo nawasihi wanawake jitokezeni kwa wingi kuwania nafasi za uongozi," amesema Kabaka.

"Wale ambao mtajitokeza kugombea nafasi hizi za uongozi pia mjitathmini mtazifanyia nini jumuiya zenu pamoja na Chama, na kujihoji kama una sifa zote za kuwa kiongozi ndipo uchukue fomu, lengo ni kupata viongozi wazuri," ameongeza.

Aidha, amesisitiza pia kwenye chaguzi hizo za viongozi, kuwepo na haki sawa kwa watu wote, wala kusiwepo na figisu figisu pamoja na kupanga safu za viongozi, bali haki itendeke ili kila mmoja apate haki yake.

Katika hatua nyingine Kabaka, amesisitiza wanawake wa UWT mkoani Shinyanga, siku ya uchaguzi mkuu (2025) wajitokeze kwa wingi kumpigia kura Rais Samia Suluhu Hassani ili apate ushindi wa kishindo.

Amesema uchaguzi huo mkuu wa 2025 ni wa muhimu sana, kwa sababu wasipo mpigia kura Rais Samia, ndiyo utakuwa mwisho wa mwanamke kuaminika tena Tanzania.

"Rais Samia ametuheshimisha sana wanawake, ndani ya mwaka wake mmoja wa uongozi amefanya mambo makubwa sana ya kimaendeleo hivyo anafaa kuendelea kutuongoza, "mitano tena" na tuendelee kumuunga mkono," ameeleza Kabaka.

"Tuendelee kuyasema yale yote mazuri ambayo Rais Samia ametekeleza, kuanzia kwenye Kata zetu ," ameongeza.

Naye Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko, akizungumza kwenye mkutano huo, amempongeza Rais Samia Suluhu Hassani kwa kutoa fedha nyingi, ambazo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo mkoani Shinyanga ikiwamo na ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa UWT mkoani Shinyanga Magreth Cosmas, amesema Jumuiya imekuwa ikihamasisha wanawake wajitokeze kwa wingi kuwania nafasi za uongozi, ambapo katika uchaguzi wa matawi na mashina wamefanya vizuri na wengi wamekuwa viongozi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Gaudensia Kabaka akizungumza kwenye mkutano na wanawake wa UWT mkoani Shinyanga.
Mwenyekiti wa UWT mkoani Shinyanga Magreth Cosmas akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Jasinta Mboneko akizungumza kwenye mkutano huo wa UWT.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye mkutano huo wa UWT.
Katibu wa UWT Mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akisoma Taarifa ya UWT mkoani humo.
Wanachama wa UWT Mkoani Shinyanga wakiwa kwenye mkutano wa Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mkutano wa UWT mkoani Shinyanga ukiendelea.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka, akitoa Kadi kwa wanachama wapya ambao wamejiunga na Jumuiya hiyo mkoani Shinyanga.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Zoezi la utoaji kadi kwa wanachama wapya wa UWT likiendelea.
Wanachama wapya wa UWT wakila kiapo.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka, akipokea zawadi ya vitu mbalimbali kwa wanachama wa UWT mkoani Shinyanga kama ishara ya upendo kwake.
Zawadi zikiendelea kutolewa.
Zawadi zikiendelea kutolewa.


Zawadi zikiendelea kutolewa.


Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala akiongoza zoezi la utoaji zawadi ya vitenge kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka.
Mwenyekiti wa UWT mkoa wa Shinyanga Magreth Cosmas naye akiongoza zoezi la utoaji zawadi ya vitenge kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka.
Katibu wa UWT mkoa wa Shinyanga Asha Kitandala, akimpatia Zawadi ya Vitenge Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka akiwa amebeba zawadi ya vitenge.
Burudani zikiendelea kwenye mkutano huo.
Burudani zikiendelea kutolewa kwenye mkutano huo.
Picha ya pamoja ikipigwa
Zoezi la upigaji picha ya pamoja likiendelea.
Zoezi la upigaji picha ya pamoja likiendelea.
Zoezi la upigaji picha ya pamoja likiendelea.
Awali Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka, akivalishwa Skafu mara baada ya kuwasili mkoani Shinyanga katika ziara yake ya kikazi.
Mwenyekiti wa UWT Taifa Gaudensia Kabaka, akiendelea na ziara yake ya kikazi mkoani Shinyanga ikiwamo kufanya mkutano pamoja na kutembelea jengo la uwekezaji la UWT mkoani Shinyanga lililopo Mkabala na Ofisi ya TRA mkoani Shinyanga.


Na Marco Maduhu, SHINYANGA.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments