TANESCO SIMIYU KUANZA KUTUMIA HUDUMA YA NI-CONEKT KUHUDUMIA WATEJA WAPYA

Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu  Alistidia Clemence

Na Samirah Yusuph - Simiyu

Shirika la umeme (TANESCO) Mkoa wa Simiyu limeanza kutumia mfumo wa kielektroniki wa Ni-konekt kupitia komputa na simu za mkononi ili kurahisisha huduma kwa wateja wapya pamoja na kupunguza msongamano wa gharama na muda wanapohitaji huduma za kuunganishiwa umeme.


Akizungumza na mafundi umeme wanaotandaza mfumo wa umeme majumbani Meneja wa TANESCO Mkoa wa Simiyu  Alistidia Clemence amesema mfumo huo utaanza kutumia ifikapo Juni 6, 2022, ambapo wateja watakuwa hawana usumbufu wa kufika ofisi za tanesco watatuma maombi popote walipo.


"Kikubwa tunachosisitiza ni kwamba wateja wakamilishe kutandaza mfumo wa umeme majumbani kabla ya kutuma maombi ili iwe rahisi na haraka kupata huduma kwa sababu mfumo huu hauna mzunguko mrefu kama ilivyokuwa awali",amesema.


"Faida za mfumo huu ni kurahisisha na kuondoa vishoka ambao walikuwa mtu kati katika utoaji wa huduma kwa wateja na itaondoa Ile usumbufu na gharama za mteja kuja na kurudi katika ofisi zetu ili kukamilisha huduma za usafiri",amesema. 


Aidha ameongeza kuwa mfumo huu hauna mzunguko na masharti mengi kama ilivyokuwa mwanzo, kwa sasa mteja atatakiwa kuwa amekamilisha kutandaza mfumo wa umeme nyumbani pia kuwa na aina yeyote ya simu ya mkononi au komputa ili kupata huduma hii na itachukua siku mbili hadi tatu ili mteja kuwashiwa umeme.


Mhandisi Johansen Mukulasi akimwakilisha mhandisi mkuu wa ufundi amesema wanachokisisitiza kwa mafundi ni ufanisi na kuhakikisha wanakizi vigezo vya usajili kutoka mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ili wakidhi kutoa huduma hizo kwa wateja.


Hapo awali mfumo uliotumika ulitaka mteja kutembelea ofisi za tanesco Ili apate fomu ya maombi kisha aanze kufuatilia usajili na ilichukua siku 30 Hadi 90 Ili mteja kuwashiwa umeme Hali iliyodababisha wateja kushindwa kupata huduma Kwa wakati.


"Ilikuwa mteja ili apate umeme ni lazima afike ofisi za tanesco na muda mwingine arudi bila kuhudumiwa kwa sababu ya changamoto za mtandao na pengine akimaliza itachukua muda mrefu Hadi kuwashiwa umeme Hali iliyodababisha sisi mafundi tuonekane matapeli", amesema Joseph Ikombe fundi umeme.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments