NAIBU WAZIRI MASANJA AKUTANA NA WATENDAJI WA KAMPUNI YA REO YA HONGKONG YA UTANGAZAJI WA MAENEO YA UWEKEZAJI


Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) akizungumza na watendaji wa kampuni ya REO Communications kuhusu kutangaza maeneo ya uwekezaji ya kitalii jijini Dodoma leo.




***********************

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Mary Masanja (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na watendaji wa Kampuni ya REO Communications kutoka Hongkong inayojishughulisha na utangazaji wa maeneo ya uwekezaji ya nchi mbalimbali barani Afrika kwa njia ya majarida.

Kikao hicho kimefanyika leo Juni 29, 2022 katika Ofisi za Wizara ya Maliasili na Utalii jijini Dodoma.

Mhe. Masanja amewapongeza watendaji hao kwa nia nzuri ya kutaka kutangaza maeneo ya uwekezaji pamoja na vivutio vya utalii vya Tanzania.

Aidha , ameahidi kutoa ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha wanafanikiwa katika adhima hiyo.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya REO Communications nchini Tanzania, Xhovana Kelmendi alisema lengo ni kuhakikisha wanatangaza maeneo ya uwekezaji katika sekta mbalimbali ikiwemo Utalii, Kilimo na Madini.

Amesema wameshafanikiwa kutangaza maeneo ya uwekezaji katika nchi ya Indonesia na wana miradi ya aina hiyo ambayo inaendelea katika nchi za Kuwait, Morocco, Nigeria, Malta na Tokyo.

Kikao hicho ni mwendelezo wa vikao vya kukutana na wadau wa Sekta ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments