MWENYEKITI UWT NJOMBE AFANYA ZIARA YA KIKAZI WILAYANI LUDEWA


Mwenyekiti wa jumuiya ya umoja wa wanawake Tanzania (UWT) mkoa wa Njombe Scolastika Kevela,ameagiza wanachama na wanawake wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kuacha kupanga safu ya uongozi badala yake watende haki katika chaguzi za ndani zinazoendelea nchini na katika mkoa huo.



Bi. Scolastika Kevela ametoa agizo alipokutana na viongozi wa jumuiya hiyo katika ziara yake aliyoifanya katika wilaya ya Ludewa ili kutoa maelekezo mbalimbali juu ya Chama na Jumuiya.


“Katika chaguzi tunazoendelea nazo,tuache kupanga safu kwasababu ukiona mtu anafanya hivyo maana yake mtu huyo hajiamini na kwa muda wote hajafanya kazi akisubiri nyakati za uchaguzi,kiongozi wa namna hiyo ni kumpiga chini”, amesema Scolastika Kevela


Aidha Bi. Kevela ametoa wito kwa wananchi na wanawake wa mkoa huo kuendelea kulea familia kwa bidii ili kuondokana na utapiamlo kwa kuwa mkoa huo upo imara kiuchumi.


“Tukalee familia zetu kwa bidii ili tuondokane na mdudu anayeitwa utapiamlo na kama sio wewe basi ukimwona jirani yako mwambie”,alisema Bi. Kevela


Baadhi ya wanawake akiwemo Ester Mwalongo na Reinihada Tweve wamekiri kuwa nyuma katika masuala ya malezi kwa watoto na kusababisha utapiamlo kutoakana na kuwa bize katika kazi huku wakiwa na uchumi mzuri.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments