MWANASIASA AUAWA KWA KUKATWA KICHWA

 Watu wenye silaha Kusini Mashariki mwa Nigeria wamemuua kwa kumkata kichwa mwanasiasa mwingine katika jimbo la Anambra.


Msemaji wa polisi, Ikenga Torchukwu ameiambia BBC kuwa mwili wa Nelson Achukwu- mbunge wa zamani katika jimbo la Anambra ulipatikana Jumanne baada ya kutekwa nyara kutoka nyumbani kwake mapema mwezi huu.

Haijabainika ni nani aliyetekeleza utekaji nyara na mauaji ya mwanasiasa huyo mlemavu.

Ripoti zinaonyesha kuwa ilikuwa ni mara ya pili yeye kutekwa nyara katika miezi kadhaa na pesa ililipwa ili kuachiliwa wakati wa kutekwa nyara kwake mara ya kwanza.

Achukwu alikuwa mwanasiasa wa hivi karibuni kulengwa katika eneo hilo.

Mamlaka mara nyingi zimewalaumu watu wanaotaka kujitenga wanaodai jimbo lililojitenga la Biafra kwa ghasia zinazozidi kuwa mbaya kusini mashariki mwa Nigeria.
 
SOMA HAPA ZAIDI CHANZO BBC SWAHILI.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments