DKT. ASHATU AITAKA CARMATEC KUFANYA UTAFITI WA MAHITAJI YA WADAU


Mhandisi Fredy Magamba kutoka kituo Cha zana za kilimo a teknolojia vijijini (CAMARTEC ) wa kwanza kulia akimuonyesha waziri wa uwekezaji , viwanda na biashara Dkt Ashatu Kijaji moja ya mashine waliobuni ya kuoteshea mahindi ,maharage na mazao mengine. 

Na Rose Jackson,Arusha


Waziri wa Uwekezaji ,Viwanda na Biashara Dkt. Ashatu Kijaji amekitaka kituo cha zana za kilimo na teknolojia vijijini (CAMARTEC)wafanye utafiti unaozingatia mahitaji ya wadau kwa kutengeneza mashine ambazo zinaweza kumsaidia mkulima kutatua matatizo katika kilimo.


Aliyasema hayo jana wakati alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho na kujionea kazi mbalimbali ambazo wanazifanya ambapo pia alitumia nafasi hiyo kuwataka wahandisi wa kituo hicho kuongeza kasi ya kubuni na kutengeneza mashine izo ili kuweza kumsaidia mwananchi ambaye ni mkulima .


Alisema watanzania wapo tayari kuona katika eneo la kilimo kunaimarika katika mnyororo mzima wa dhamani tangu wanapopanda hadi wanapo vuna hivyo ni vyema wakaendelea kutengeneza vifaa ambavyo vitamsaidia mkulima


Alibainisha kuwa zaidi ya asilimia 75% ya watanzania ni wakulima hivyo wakiweza kufanya zaidi wataweza kuwanufaisha watanzania .

“Awali kituo hichi mlikuwa mnalalamika hampati bajeti lakini sasaivi serikali ya Rais samia imewaletea bajeti lakini hamuitumii tunashidwa kuwaelewakwanini haimtumii hizi ela kwa ajili ya malengo mme lala sana sasa nataka kuwaambia muamke muanze kukimbi serikali ya mama samia aina shida ya fedha bali inashida ya wataaalam ambao wanafanya kazi kwa kasi “alisema Dkt. Ashatu.

Alisema kuwa taifa linaitaji viwanda vingi vidogovidogo ili kuweza kuwasaidia wananchi haswa wakulima na wafugaji hivyo wajitaidi kubuni zaidi mashine zitakazo saidia

“Mkibuni msiishie kubuni tu bali mbuni na mvitangaze muende hadi vijijini mkazitangaze mashine hizo kwa wakulima ili wakulima wajue nyie kama CAMARTEC mnafanya nini “alisema Dkt. Ashantu



Kwa upande wake Kaimu mkurugenzi mkuu wa kituo hicho Pythias Ntella alisema kuwa taasisi hiyo ina umuhimu mkubwa sana katika mapinduzi ya Viwanda na Kilimo ili kufikia kilimo chenye tija kwa ajiri ya ukuaji wa Uchumi wa viwanda hivyo wata jitaidi kufanya kazi kwa kasi ili kuweza kuwafikia Wananchi kwa haraka.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments