MKE AMKATA MMEWE SEHEMU ZA SIRI KWA WEMBE

 Picha haihusiani na habari hapa chini

****


Jeshi la Polisi mkoani Ruvuma linamshikilia Mwanamke mmoja ajulikanaye kwa jina la Hellen Mchahuru (40) kwa tuhuma za kumjeruhi kwa kumkata na wembe sehemu za siri (Korodani ya kushoto) mumewe Vintan Luhiva (42).

Kamanda wa Polisi mkoa wa Ruvuma Joseph Konyo  amesema mtuhumiwa aliweza kufanya tukio hilo wakati mwanaume huyo akiwa amesinzia.

ameeleza kuwa mtuhumiwa alichukua wembe na kumjeruhi kwa kumkata korodani moja upande wa kushoto na kumsababishia maumivu makali.

Kamanda Konyo amesema majeruhi amelazwa kwenye hospitali ya Wilaya ya Tunduru akipatiwa matibabu na kwamba mtuhumiwa anayedaiwa kutenda tukio hilo yupo mikononi mwa Polisi na hatua za kumpeleka Mahakamani zinafuata baada ya hatua za upelelezi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post