DIRISHA LA USAJILI KWA KLABU ZA LIGI KUU YA NBC, CHAMPIONSHIP, FIRST LEAGUE KUFUNGULIWA JULAI 2Afisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo.

**
Dirisha la usajili kwa Klabu za Ligi Kuu ya NBC, Championship, First League na Ligi Kuu ya Wanawake ya Serengeti Lite msimu wa 2022/2023 litafunguliwa Julai 1, 2022 na kufungwa Agosti 31, 2022.


Katika kipindi hicho Klabu zinatakiwa kukamilisha usajili na uhamisho wa Kimataifa.

Klabu zote zinapaswa kuzingatia muda huo wa usajili, hakutakuwa na muda wa ziada baada ya dirisha kufungwa. Yeyote atakayekutana a changamoto awasiliane na Idara ya Mashindano TFF.

Aidha Dirisha Dogo lenyewe litafunguliwa Desemba 16, 2022 na kufungwa Januari 15, 2023.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post