WATU WATATU HOI HOSPITALI BAADA YA KULA NYAMA YA NG'OMBE MGONJWA

Watu watatu wamelazwa katika Hospitali ya Shibwe, eneo bunge la Ikolomani, Kaunti ya Kakamega nchini baada ya kula nyama kutoka kwa ng’ombe aliyekuwa na ugonjwa.

Afisa wa kliniki wa hospitali hiyo Brian Angadi alithibitisha kisa hicho akisema kuwa watatu hao walikuwa nyama kutoka kwa ng’ombe aliyekuwa na ugonjwa wa kimeta maarufu kama anthrax.

 Kimeta ni ugonjwa hatari wa kuambukizana ambao kawaida huathiri mifugo na wanyama wa msituni duniani kote. 

“Watatu hao walipatikana na ugonjwa wa kimeta. Tulifanya kila juhudi kuwatibu na tukafanikiwa kuwatoa kwenye hatari,” Angadi aliambia gazeti la the Standard.

Hata hivyo ameonya uwezekano wa kupokea wagonjwa zaidi kwa kuwa wakaazi wengine wa kijiji hicho walipata mgao wa nyama hiyo.

Akizungumzia kisa hicho, Gilbert Mukumba, mmoja wa wagonjwa ambaye tayari ameruhusiwa kwenda nyumbani alisema kuwa aliitwa na marafiki zake watatu kwenda kusaidia kuchinja ng’ombe na angepewa nyama ya bwerere kama malipo. 

Aliichukua nyama hiyo na kuipeleka familia yake nyumbani lakini wiki moja baadaye alianza kufura mikono na mwili wake kudhoofika. 

“Nilianza kushuhudia majibu kwenye ngozi yangu na mengine yaliyoumba sana kwenye mikono na miguu. Nilitumia dawa ya kitamaduni lakini haikusaidia. Nilipoenda hospitalini madaktari waliniambia kuwa nilikuwa nimekuala nyama kutoka kwa ng’ombe aliyekuwa na ugonjwa,” alisema. 

Wakaazi wamehimizwa kukimbia hospitalini iwapo wataanza kushuhudia dalili za ugonjwa wa kimeta katika miili yao.

Chanzo - Tuko News 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post