NBS YASAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA KOREA KUSINI KUKUSANYA NA KUZALISHA TAKWIMU...WALIMU WA WALIMU WAPEWA MAFUNZO YA SENSA

Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa (kushoto) na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini. Kulia ni Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Ofisi ya Taifa ya Takwimu nchini Tanzania (NBS) imesaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini ambapo Taasisi hiyo ya Korea Kusini itaisaidia NBS kujenga uwezo wa kukusanya na kuzalisha takwimu.

Chini ya ushirikiano huo, NBS watapatiwa mafunzo katika nyanja mbalimbali humu nchini na nchini Korea Kusini, Kompyuta 80 na kuimarisha maabara ya Teknolojia ya habari ya NBS.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo Jumanne Juni 14, 2022 na Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakati wa Mafunzo kwa walimu wa walimu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 yanayoendelea katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Dkt. Chuwa ameeleza kuwa Serikali ya Korea Kusini imetoa msaada wa Vishikwambi (Tablets) 10,000 na Kompyuta za kawaida 50 na Kompyuta mpakato (Laptops) 30 kwa ajili ya kukusanyia takwimu katika Sensa ya Watu na Makazi 2022.

“Tunaishukuru Korea Kusini wamekuwa wadau wakubwa wa maendeleo, tumeanza ushirikiano nao tangu mwaka 2014 na leo tumekuja kusaini makubaliano ya kutoa elimu kwa kutumia teknolojia. Kwa upande wa Afrika nchi ya Tanzania imekuwa nchi ya kwanza kufikiwa na hawa wenzetu kutoka Korea Kusini”,amesema Dkt. Chuwa.

Katika hatua nyingine Mtakwimu Mkuu wa Serikali amesema maandalizi ya Sensa ya Watu na Makazi ya 2022 yanaendelea vizuri ambapo tayari wanaendelea kutoa mafunzo kwa wadau mbalimbali wakiwemo waandishi wa habari wa mitandao ya kijamii, Redio za Kijamii na Walimu 400 ngazi ya taifa watakaokwenda kutoa elimu katika ngazi mbalimbali kuanzia mikoa.

Kwa upande wake Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar amewahamasisha wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi litakalofanyika Agosti 23,2022.

Naye Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazofanya vizuri katika masuala ya takwimu na kwamba Korea Kusini itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika utoaji elimu kwa njia ya teknolojia ya habari ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa mbalimbali vya kidigitali.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa (kushoto) na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakisaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini leo Juni 14,2022 katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa ambapo Taasisi hiyo ya Korea Kusini itaisaidia NBS kujenga uwezo wa kukusanya na kuzalisha takwimu. Kulia ni Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa (kushoto) na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakisaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa (kushoto) na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakibadilishana nyaraka baada ya kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini. Kulia ni Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa (kushoto) na Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo wakionesha nyaraka baada ya kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini. Kulia ni Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar
Mtakwimu Mkuu wa Serikali ya Tanzania Dkt. Albina Chuwa akizungumza wakati wa hafla fupi ya NBS kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini 

Meneja Mradi kutoka Ofisi ya Takwimu nchi ya Korea Kusini Bwana Charlie Seo akizungumza wakati wa hafla fupi ya NBS kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini 

Kaimu Mtakwimu Mkuu wa Serikali, Zanzibar , Bi. Mashavu Khamis Omar Viongozi akizungumza wakati wa hafla fupi ya NBS kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini 
Viongozi wakiwa hafla fupi ya NBS kusaini Mkataba wa ushirikiano na Ofisi ya Takwimu ya nchi ya Korea Kusini 

Walimu wa walimu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 wanaoendelea na mafunzo wakiwa katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa

Walimu wa walimu wa Sensa ya Watu na Makazi 2022 wanaoendelea na mafunzo wakiwa katika Ukumbi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa Iringa.

Picha zote na Kadama Malunde - Malunde 1 blogDownload/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post