JAMAA ALIYEKIRI KUIBA KANISANI AIOMBA MAHAKAMA IMRUHUSU ATUBU KWANZA KABLA YA KWENDA JELA


Mwanaume mmoja aliyeiba vifaa vya kielektroniki kutoka kwa kanisa moja mjini Eldoret nchini Kenya ameomba mahakama imruhusu atubu.

Kijana huyo mwenye umri wa miaka 18 aliyekiri kuiba ala za kanisa la Kenya Assemblies of God (KAG) aliitaka mahakama kumruhusu kuomba msamaha kutoka kwa uongozi wa kanisa hilo kabla ya kufungwa jela.

Katika ripoti ya Daily Nation, mshtakiwa, John Kiiru ambaye anadaiwa kuiba vifaa vya muziki, alisema pia anataka kukombolewa kabla ya kwenda jela. 

Mshukiwa alimwambia hakimu wa mahakama ya Eldoret Dennis Mikoyan, anataka kutumia kifungo chake gerezani kuwahubiria wafungwa wengine baada ya kugeuzwa kuwa ‘Kuzaliwa kwa mara ya pili katika Kristo’.

"Nimejutia sana nilichofanya, naomba mahakama hii inisaidie kumfikia pasta wa kanisa na viongozi wengine kuomba msamaha kabla ya kuhukumiwa," aliiambia mahakama wakati akihukumiwa.

 Kesi hiyo itatajwa Juni 27 kwa ripoti ya uangalizi ili kubaini aina ya hukumu ambayo mahakama itampa mshtakiwa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post