MWANAFUNZI AUAWA, ATOBOLEWA JICHO NA KUPONDWA UNYAYO

Mwili wa mtoto Johnson Thomas (14) mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Buhalahala mjini Geita aliyeuawa.

**
Mtoto Johnson Thomas (14) mwanafunzi wa darasa la saba katika Shule ya Msingi Buhalahala mjini Geita amekutwa amefariki dunia na mwili wake kutupwa pembeni ya mto karibu na Barabara ya Buhalahala kwenda Kijiji cha Nyakato.


Tukio la mtoto huyo kuuawa ni tukio la tatu ndani ya wiki mbili ambapo watoto wengine wawili mmoja akiwa na miaka miwili aliuawa kwa kukatwa shingo na mwingine wa miaka saba inadaiwa alilawitiwa na kubakwa kisha kukatwa shingo wilayani Nyang’hwale mkoani humo.

Jeshi la Polishi Mkoa wa Geita limesema linaendelea kuchunguza tukio la mauaji ya mtoto Johnson Thomas  ambaye mwili wake umekutwa pembeni ya mto Mita 120 kutoka barabara inayotoka Buhalahala senta kuelekea Kijiji cha Nyakato Mjini Geita.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Kamishna Msaidizi wa Jeshi la Polisi Henry amesema kuwa uchunguzi wa awali umebaini kuwa mtoto huyo alitoka nyumbani kwao kwa kutumia Bajaj iliyokuwa inaendeshwa na Benson Theophili Juni 12,2022 majira ya saa 11 jioni.


Ameeleza kuwa mtoto huyo alikuwa alikuwa anaelekea senta kushona sare zake za shule na mara ya mwisho alionekana na Mwanafunzi mwenzake (jina limehifadhiwa)akielekea barabara ya zilipo ofisi za Kampuni ya GPH.


Mwaibambe ameeleza kuwa mtoto huyo hakuonekana tena mpaka alipokutwa amefariki Juni 18,2022 na eneo la tukio linaonyesha mwili huo uliletwa hapo.


Amefafanua kuwa mwili wa marehemu baada ya uchunguzi ulibainika kuwa na majeraha mguu wa kushoto ukiwa umepondwa na kitu kizito na jicho kuumizwa na kugeukia ndani.


Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments