ANUNUA JENEZA JIPYA LA MILIONI 1.2 AKIJIANDAA NA MAZISHI YAKE...ALISHANUNUA MENGINE MAWILI



Mzee mmoja kutoka kaunti ya Busia nchini Kenya amewaacha wenyeji vinywa wazi baada ya kujinunulia jeneza la tatu.

Alloise Otieng' Ominang'ombe mwenye umri wa miaka 87 amenunua jeneza jipya la thamani ya KSh 58,000  sawa na shilingi 1,218,000 za Tanzania na ambalo anatazamia kutumia kama gari lake la mwisho duniani.

Mzee huyo anatoka katika kijiji cha Kajoro huko Okatekok, eneo bunge la Teso Kusini kaunti ya Busia.

 Alikuwa amenunua majeneza mengine mwaka 2009 na 2012; hata hivyo alisema yalikuwa yamepitwa na wakati ikilinganishwa na mtindo wa sasa wa kuunda majeneza.

Aliambia runinga ya Citizen kwamba majeneza ya awali yatapasuliwa kuwa vipande vya kuni wakati wa mazishi yake, huku lile alilonunua jipya likitumika katika kumzika.

 "Mawili hayo yatapasuliwa vipande vipande ili vitumike kupika wakati wa mazishi yangu," alisema.

“Nataka hili liwe funzo kwa jamii yangu kwa ujumla. Unaweza kukosa mahitaji ya msingi ukiwa hai. Lakini ukifa, watu watachinja ng'ombe, watakununulia nguo nzuri na viatu wakati utakuwa umeenda kabisa. Ndiyo maana niliamua kupanga jinsi safari yangu ya mwisho itakavyokuwa inayolingana na hadhi yangu katika jamii,” aliongeza.

Katika taarifa sawia na hiyo aliyeishiwa nguvu huko Suna, kaunti ya Migori, jamaa aliyeonekana kuchoshwa na maisha alinunua jeneza nyeupe na buluu, na kulipeleka nje ya nyumba yake kisha akaingia na kujilaza ndani. Mzee huyo aliwaacha wengi vi nywa wazi wakishangaa ni vipi aliamua kufanya kitendo hicho cha ajabu.

Kulingana na Awino, alikuwa amechoshwa na mizozo ya kila mara baina yake, mkewe na wanawe na ndiposa akaamua kufanya kisa hicho cha kustaajabisha.

Akiwa amelewa kabisa, baba huyo wa watoto watatu alishtumu familia yake kwa kumsukuma ukutani huku akisema kila mara alitaka kujitoa uhai. Majirani zake walishtuka, wakatoka nje ya boma hilo mara moja na kurudi baadaye kumsihi Awino asijiue.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments