CHONGOLO AANZA ZIARA YA KICHAMA NCHINI BURUNDI

 
Katibu Mkuu wa CCM Daniel Chongolo (katikati) akizungumza na waandishi wa Habari mbele ya viongozi wa CCM mkoa Kigoma (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa CCM mkoa Kigoma Amandus Nzamba.


Na Fadhili  Abdallah, Kigoma
KATIBU Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameanza ziara ya kichama  Nchini Burundi Kwa lengo la Kuimarisha Uhusiano Baina ya Chama Tawala Cha Burundi (CNDD FDD) Na CCM ambapo pamoja na mambo mengine atatembelea uwanja wa michezo na kituo cha kukuza vipaji kwenye mkoa wa Makamba nchini Burundi 

 

Chongolo Alisema hayo katika uwanja wa ndege wa Kigoma majira ya saa 11 jioni 

alipowasili Mkoani Kigoma  akiwa  njiani  kuelekea Nchini Burundi akiongozana na Viongozi wengine wa chama hicho Taifa, Wilaya na Mkoa Kigoma, ambapo alitarajia  kupokelewa na Wenyeji wake Mpakani mwa Tanzania na Burundi Manyovu Wilaya ya Buhigwe Mkoani Kigoma jioni leo.

 

Katika Ziara yake Nchini Burundi Katibu mkuu Chongolo atakagua Uwanja wa Mpira uliojengwa Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, ambao unaomiklikiwa na Katibu Mkuu wa CNDD-FDD, Reverien Ndikuriyo uwanja huo pia una kituo cha kukuza vipaji.


Alisema kuwa uwanja huo  utakuwa chachu katika kuibua vipaji kwa wanamichezo nchini  Burundi lakini pia itajuwa fursa kubwa kwa Watanzania kutumia nafasi hiyo kwa wanamichezo wake kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanamichezo wake chipukizi hasa wa mkoa Kigoma.



 

“MKOA wa Kigoma Unahitaji kupata timu ya ligi kuu kwa hio huu ushirikiano kati ya Tanzania na Burundi Kupitia Michezo, utakuwa mwanzo mzuri wa kufanikisha mkoa Kigoma kuwa na timu ya ligi kuu kwenye soka sambamba na michezo mingine,"alisema Chongolo


aliongeza Kuwa Mkoa wa Kigoma Una vipaji Vingi na kwamba kutakuwa na mwendelezo wa ligi itakayohusisha mikoa ya Burundi na Mkoa wa Kigoma kwa lengo la kuibua vipaji, na kuwezesha ajira na kujenga afya kupitia michezo na vijana wengi wakae mkao wa kula burudani kupitia michezo.

 

Aidha aliongeza kuwa Kukamilika kwa Uwanja wa Mpira Wa Makamba nchini Burundi ni chachu kwa Chama hicho kuboresha uwanja wake wa Lake Tanganyika uliopo mkoani Kigoma wa kuendeela kuboresha ili kuweka uwiano wa viwanja vitakavyo endelea kukidhi mahitaji muhimu ya kimichezo kwa nchi hizo na ligi za ndani.


Uwanja huo pia ndiyo uwanjani wa nyumbani na makao makuu ya timu ya Eagle Noir (Black Eagle) inayocheza ligi kuu ya nchini Burundi

 

Katibu Mkuu wa CCM anatarajia kufika Bujumbura nchini Burundi ambapo atakuwa na mazungumzo na viongozi wa CNDD- FDD.


Alisema kuwa ziara hiyo inafanyika kwa Mwaliko wa Katibu Mkuu wa CNDD- FDD ambaye ameshafanya ziara mara tatu nchini Tanzania.

 




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments