WATANZANIA WATAKIWA KUYATUMIA MAKUMBUSHO KWA KULETA AJIRA NA KUJIFUNZA

Mkurugenzi wa makumbusho ya Azimio la Arusha Drt Gwakisa Kamatula akiwa pamoja na mgeni rasmi Mchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki na wageni wengine katika siku ya maadhimisho ya makumbusho duniani yaliyofanyika viwanja vya Azimio la Arusha .

Na Rose Jackson,Arusha

Watanzania wametakiwa kuyatumia Makumbusho kama njia mojawapo ya kuleta ajira na kujifunza Ikiwa ni pamoja na kuwa kielelezo muhimu katika historia ya nchi kwani yamebeba historia kubwa ya nchi ya Tanzania.


Hayo yamesemwa na Mchumi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Valeriani Vitalis wakati akiwa mgeni Rasmi katika kilele cha siku ya Makumbusho duniani yaliyofanyika katika viwanja vya Makumbusho ya Azimio la Arusha yenye kauli mbiu isemayo 'Nguvu ya makumbusho katika kuelimisha na kuburudisha jamii'.


Amesema makumbusho yanaweza kuleta ajira kwani yana historia na elimu mbalimbali ambazo zina uwezo wa kuwafanya watanzania kuweza kujifunza na kujiajiri.


Ameeleza kuwa maeneo ya makumbusho yamesheheni historia mbali mbali za Taifa hivyo yanahitaji maboresho makubwa yanayo paswa kwenda na wakati ili yaweze kuvutia watalii kutoka ndani na nje ya nchi.

Aidha amesema amefurahishwa na maboresho yanayoendelea katika Makumbusho hayo na kuongeza kuwa Makumbusho yakiboreshwa yatasaidia kuunga mkono kwa vitendo juhudi za baba wa Taifa Mwalimu Julius kambarage nyerere katika kutunza na kuenzi utamaduni wa Taifa.

Kwa upande wake mkurugenzi Makumbusho ya Azimio la Arusha Dkt. Gwakisa Kamatula amesema makumbusho ni sehemu sahihi ya kuwarisisha na kuwafundisha vijana kuhusiana na masuala mbalimbali ya kijamii kisiasa na kiuchumi.


Dkt Gwakisa ametoa rai kwa watanzania kutembelea makumbusho yaliyopo nchini ili kuweza historia na kujifunza urithi wa asili tuliorithi kwa vizazi vilivyotangulia nchi.


Kwa upande wao baadhi ya washiriki walioshiriki katika makumbusho hayo wamesema kupitia maadhimisho hayo wameweza kujifunza historia na elimu mbali mbali za makumbusho ya Taifa.


Maadhimisho hayo yamehudhuriwa na wanafunzi wa ngazi mbalimbali kwa lengo la kujifunza na kujionea historia ya Taifa la Tanzania.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post