SHULE YA SEKONDARI ILIYOSHIKA NAFASI YA TATU KITAIFA WAMSHUKURU RAIS SAMIA KUWABORESHA MIUNDOMBINU YA ELIMU, SHAKA ATIA NENO


Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la maji ndani ya moja ya chumba cha Maabara shule ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara jana Mei 15,2022.

Na Said Mwishehe, Michuzi TV

SHULE ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara ambayo imeshika nafasi ya tatu kitaifa matokeo ya kidato cha nne mwaka 2021 wameishukuru Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuboresha miundombinu ya shule yao, hivyo kufanya shule kimasomo.


Wametoa salamu hizo za shukrani kwa Rais Samia na Serikali yake kupitia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Shaka Hamdu Shaka ambaye alifanya ziara ya kuitembelea shule hiyo kwa lengo la kuwapongeza na kuwafikisha salamu za Rais Samia kuwa ataendelea kuboresha miundobinu ya sekta ya elimu nchini.

Mkuu wa Shule hiyo Stephene Naman amemueleza Shaka kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inastahili pongezi na shukrani kwa kuendelea kuboresha miundombinu ya shule hiyo , hivyo kwa kipekee wanamshukuru Rais Samia.

“Taaluma ya wanafunzi shuleni kwetu imekuwa ikimarika na kuridhisha mwaka hadi mwaka kwani mwaka 2021 shule ilikuwa na ufaulu wa daraja la kwanza hadi daraja la tatu tu katika matokeo ya mtihani wa taifa kidato cha nne mwaka jana.

“Katika matokeo ya mtihani jumla ya wanafunzi waliofanya mtihani walikuwa 95, waliopata daraja la kwanza ni wanafunzi 29,daraja la pili wanafunzi 54 na daraja la tatu walikuwa 12.Hakuna daraja la nne wala zero.

“Kwa matokeo hayo tumefanikiwa kuwapeleka wanafunzi 83 ngazi ya kidato cha tano na wanafunzi 12 vyuo vya kati.Mafanikio yetu yanatokana na jitihada za Serikali kuboresha miundombinu yetu hapa shuleni,”amesema.

Akifafanua zaidi, amesema shule yao imepata tuzo mbili kutoka Wizara ya TAMISEMI kwa kushika nafasi ya tatu kitaifa kwa shule za kata na nafasi ya kwanza kwa shule zilizoboresha ufaulu kwa kiwango cha juu kwa miaka mitatu mfululizo.

Kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, madarasa , mabweni na bwalo , Naman amemwambia Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM kuwa ujenzi wa madarasa mawili umekamilika na mradi umegharimu Sh.46,576,140 .

Pia wamekamilisha mabweni mawili kwa ajili ya kidato cha tano na sita yaliyogharimu Sh.425,960,262.Aidha ujenzi wa maabara mbili na darasa moja yaliyogharimu Sh.189,294,600 pamoja na ujenzi wa bwalo ambalo limegharimu Sh.248,960,651.

Kwa upande wake Shaka pamoja na kupata taarifa kuhusu shule hiyo amepata fursa ya kukagua ujenzi wa miundombinu ambapo amewaleza wananchi kinachofanywa katika shule hiyo pamoja na shule nyingine ni sehemu ya utekelezaji wa Ilani ya CCM.

Shaka amesema Ilani ya CCM inaelekeza kwa Serikali kuhusu kuboreshwa kwa miundimbinu ya elimu katika sekta ya elimu.Aidha amewapongeza walimu na wanafunzi kwa shule hiyo kuwa na ufaulu mzuri ambapo ametoa mwito kwa wanafunzi kuhakikisha wanajikita zaidi kwenye masomo kwani Serikali imetimiza wajibu wake.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akifungua bomba la maji ndani ya moja ya chumba cha Maabara shule ya Sekondari ya Ayalagaya iliyopo mkoani Manyara jana Mei 15,2022.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akipokea taarifa ya shule kutoka kwa Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya, Stephene Naman

Muonekana wa madarasa mawili ambayo tayari yamekamilika

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Shaka Hamdu Shaka akimkabidhi tuzo Mkuu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya, Stephene Naman kwa kufanya vizuri Kitaifa,tuzo hiyo imetolewa kwa niaba ya CCM mkoa wa Manyara

Baadhi ya Walimu wa Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya wakiwa katika picha ya pamoja na tuzo yao

Moja ya bweni ya  Shule hiyo ya Sekondari ya Ayalagaya ambayo tayari limekamilika.PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-MMG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments