KIKAO KAZI CHA WAHARIRI NA BRELA CHAMALIZIKA MKOANI MOROGORO


Bw. Seka Kasera Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni (BRELA) akifunga Kikao Kazi kati ya Wahariri wa Vyombo vya habari na BRELA kilichokuwa kikifanyika kwenye hoteli ya Nashera mkoani Morogoro kwa siku mbili, kikao hicho kimemalizika leo Mei 22, 2022.

MKuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Elimu kwa Umma Bi. Roida Andisamile Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni (BRELA) akizungumza na kukaribisha maoni ya wahariri kuhusu Mapendekezo yao baada ya Majadiliano na Mkakati wa Ushirikiano kati ya BRELA na vyombo vya habari katika Kikao Kazi cha Wahariri wa Vyombo vya habari iliyokuwa ikifanyika kwenye Hoteli ya Nashera mjini Morogoro.

Bw. Andrew Mkapa Mkurugenzi wa Leseni Wakala wa Usajiri wa Biashara na Leseni (BRELA) akiwasilisha mada ya Majukumu ya Kurugenzi ya Leseni, Mafanikio na Maboresho kwenye utoaji wa Leseni ikiwemo Changamoto zinazotokana na utafsiri tofauti kutoka kwa Umma katika Kikao Kazi cha Wahariri wa Vyombo vya habari iliyokuwa ikifanyika kwenye Hoteli ya Nashera mjini Morogoro.Bw. Seka Kasera Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu akiwasilisha mada ya Majukumu ya Kurugenzi ya Miliki na Ubunifu kwa wahariri wa vyombo vya habari kwenye kikao kazi kinachofanyika mjini Morogoro.


Bw. Seka Kasera Kaimu Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Miliki Ubunifu akionesha moja ya bidhaa kwa wahariri wa vyombo vya habari wakati akiwasilisha mada ya Majukumu ya Kurugenzi ya Miliki na Ubunifu.


Bw. Meinrad Rweyemamu Kamimu Mkurugenzi wa Biashara na Majina ya Biashara BRELA akiwasilisha mada Kuhusu Majukumu ya Kurugenzi ya Biashara na Majina ya Biashara kwenye kikaokazi cha Wahariri wa vyombo vya habari kikachofanyika kwenye hoteli ya Nashera mjini Morogoro.


Picha zikionesha wahariri kutoka vyombo mbalimbali vya habari wakifuatilia mada katika kikao kazi kati ya BRELA na Wahariri wa vyombo vya habari kinachofanyika kwenye hoteli ya Nashera


Afisa Habari Mkuu Wakala wa Wakala wa Biashara na Leseni BRELa Theresa Chilambo akiwa na baadhi ya wahariri kushoto ni Peter Mwendapole Nipashe na Mugaya Kingoba Habari leo wakifuatilia mada katika kikaokazi hicho.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post