WANANCHI WAIPONGEZA SERIKALI KUTEKELEZA AGIZO LA WAZIRI MKUU KWA WAKATI


Dkt. legyle Vumilia kushoto akikabidhi mtambo utakaotumika kwa tiba mtandao kwa Hospitali ya mkoa Songea
Mganga mfawidhi Hospitali ya Rufaa mkoa Songea DKt Magafu majula akiwaonesha waandishi wa habari jengo la huduma la dharula ambalo limekamilika kwa asilimia miamoja na limetumia Tsh milioni 600
Kaimu mkuu wa kitengo cha mawasiliano Serikalini Wizara ya Afya Bi Catherine Sungura akiongea na waandishi wa habari (Hawapo pichani)namna Wizara ya Afya itakavyoboresha huduma za Afya Nchini kote
***

Wananchi Mkoani Ruvuma wameipongeza Wizara ya Afya kwa kutekeleza agizo lililotolewa na Waziri Mkuu Mqjaliwa kasim majaliwa alilotoa mwaka 2019 la Hospitali ya rufaa ya Mkoa Ruvuma kupatiwa vifaa vya kisasa vya tiba.


Bi. Fabiola Haule ambaye amekuwa akisumbuliwa na tatizo la ugonjwa wa moyo na hakufanikiwa kwenda mhimbili kutokana na kushindwa kupata fedha amesema sasa wamepata nafuu ya matibabu na kuomba huduma hiyo ianze mapema.

Akikabidhi vifaa vya kisasa vya tiba mtandao kwa hospitali ya rufaa ya songea Mratibu wa tiba mtandao wa wizara ya Afya Dkt Legyle Vumilia alisema vifaa hivyo vitakamilisha upatikanaji wa huduma ya matibabu ya kibingwa yatayofanyika hapa mkoani bila mgonjwa kulazimika kwenda kwenye hospitali za rufaa za kitaifa kama ilivyo sasa.


Dkt. Vumilia alisema wagonjwa wa kansa, au magonjwa ambayo huduma zake hutolewa kwenye hospitali za kutaifa Muhimbili, Ocean road, Benjamin mkapa na kwingineko watapata tiba na vipimo vyote wakiwa songea na kuungwanishwa na hospitali hizo ambapo mabingwa watawaona na kuwahudumia sawa na wale waliokuwa mhimbili na hospitali nyingine kubwa kuanzia katikati ya mwezi ujao wa sita mwaka huu 2022 huduma hiyo.


Dkt. Vumilia aliwaambia waandishi wa habari kuwa huduma hii itawasaidia pia nchi majirani zetu wa Malawi na Msumbiji ambao wamekuwa wakija kutibiwa kwenye hospitali yetu ya Rufaa ya mkoa Songea mara nyingi.


Kwa upande wake mganga mkuu mfawidhi wa Hospital ya mkoa Songea Dkt. Magafu Majura alisema tayari wataalamu watano wa hospitali hiyo wameshapatiwa mafunzo ya kutumia mashine za tiba mtandao na Daktari mmoja anamalizia mafunzo ya kibingwa na kufanya kitengo hicho kuwa na wataalamu sita ambao watakidhi mahitaji kwa sasa.

Dkt. Majura alisema Hospitali hiyo imekamirisha jengo la kisasa la wagonjwa wa dhalula na Chumba cha kisasa cha wagonjwa mahututi kikiwa na mifumo ya hewa ya Oksijeni kwa kila kitanda.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post