OFISI YA MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA YAMSIMAMISHA MBATIAMwenyekiti wa NCCR-Mageuzi James Mbatia

OFISI ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, imemsimamisha Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, James Mbatia na sekretarieti yake yote, kutojihusisha na siasa ndani ya chama hicho hadi uamuzi huo utakapoamuliwa vinginevyo.


Uamuzi huo umetolewa leo Jumatano Mei 25, 2022 na Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza akisema uamuzi wa Kikao cha Halmashauri ya chama hicho kilichofanyika Mei 21 mwaka huu, ulikuwa halali kwa akidi ya wajumbe wake licha ya kutotaja uhalali wa akidi hiyo.


Nyahoza amesema kwa mamlaka ya ofisi hiyo, inamtaka Mbatia kutojihusisha na siasa ndani ya chama hicho hadi uamuzi huo utakapotenguliwa na chama.

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Sisty Nyahoza

“Baada ya kusimamishwa, katibu wa chama hicho alituletea barua kwa fomu ya kisheria inayotujulisha kusimamishwa uanachama, tumekubaliana na uamuzi huo.

“Kama hawataridhika (Kina Mbatia) ziko njia za kutafuta haki, waende Mahakamani,” amesema Nyahoza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post