BODI YA WAKURUGENZI WA SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA (NHC) YASISITIZA KASI UJENZI WA NYUMBA DODOMA



MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),Dkt.Sophia Kongela amesema, ni shauku yao kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa na shirika hilo ikiwemo ya ujenzi wa nyumba jijini Dodoma inakamilika kabla ya muda ili kutoa nafasi katika utekelezaji wa miradi mingine nchini.
Dkt.Kongela ameyasema hayo leo Mei 19,2022 baada ya Bodi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kutembelea na kukagua mradi wa nyumba unaojengwa na shirika hilo jijini Dodoma, ambapo imesisitiza ujenzi wa nyumba hizo ufanyike kwa ubora, kiwango na muda uliopangwa kusudi ulete tija kwa nchi.


"Sisi tunashukuru kama bodi tumepata nafasi ya kuja kutembelea miradi yetu, tumeona kuna mwendelezo mzuri, kwa sababu ilivyoanza tuliona na tumeona tuko makini nini kinaendelea.


"Tumekuwa tukipata feedback (mrejesho),tumetoka chini ambako huwa kunasumbua,na kwa sasa hakuna kitu cha kutusubirisha, kuna maendeleo tunaomba muendelee kupambana na sapoti yetu mnayo shirika zima linawaangalia ninyi,"amefafanua Dkt.Kongela.
Amesema kuwa,Idara ya Uhandisi na Ujenzi ya NHC inapaswa kuendelea kutambua kuwa shirika hilo lipo nyuma yao na linawapa sapoti kuona wanafanya kazi hiyo kwa ubora na kwa muda ambao umepangwa kama ambavyo Mkurugenzi wa NHC ameomba.


Dkt.Kongela ameongeza kuwa, kukamilika kwa miradi hiyo kunatoa fursa kwa miradi mingine iliyopo jijini Dar es Salaam, hivyo akawataka kutekeleza kwa kasi kuhakikisha kwamba inafanyika kwa haraka.
"Nafikiri mmeshasikia kuna miradi mingine inakuja kule Dar es Salaam na karibuni itaanza, tegemeo letu ni ninyi kwa hiyo mjitahidi kufanya kazi kwa haraka tuweze kumaliza mapema haya majengo yetu Injinia (Mhandisi) hapa yupo,nafikiri mnaenda vizuri hakuna shida yoyote.


"Tufanye kazi kwa bidii mnasapoti yetu tunawatakia kazi njema na kila la heri tupambane ninyi bado ni vijana mnaweza,endeleeni hivyo hivyo tumalize mapema iwezekanavyo hata (DG) ameliona hilo angalau tumalize miezi sita kabla, utaleta tija kubwa kwa taifa,"amesema Dkt.Kongela.


Pia amesema, ili kasi ya ujenzi iwe kubwa wanahamasisha vifaa vya ujenzi viwe eneo la kazi na si muda wa kazi ndiyo mchakato wa manunuzi unaanza kwani kwa kufanya hivyo kutachangia kasi ya ujenzi kupungua.


Uhandisi na Ujenzi


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Uhandisi na Ujenzi wa NHC, Haikamen Mlekio amesema, wanatekeleza mradi huo katika maeneo ya Chamwino na Iyumbu jijini Dodoma.
"Miradi yetu ya ndani tunayo miwili, mmoja ni ule tuliozunguka kule wa nyumba 300 kwa awamu ya kwanza na awamu ya pili nyumba 1000 ambapo ni katika site mbili, site ya Iyumbu na site ya kule Chamwino.


"Hapa tuliposimama tunajenga nyumba 303 kwa maana majengo haya yako 300 na majengo ya huduma yako matatu, tuna Nursery, Club house pamoja na duka na katika hizi nyumba tulizokaa hapa katika hizi nyumba 1000 hizi 300 ziko za aina tatu,"amesema Bw.Mlekio.


Amefafanua kuwa, "Nyumba ziko 150 za mita za mraba 120 square mita na square mita ziko 100 na square mita 75 ziko 50 na jumla zinakuwa 300. Lakini kule tulikotoka mwanzoni kuna nyumba za aina tatu vilevile kuna nyumba zenye square mita 115, kuna nyumba zenye square mita 85, kuna nyumba zenye square mita 79, lakini ukiziangalia kwa nje ni kama ndogo, ni nyumba ambazo tunasemaga ni toroka uje, chumba kimoja kinajitegemea kwa nje kule Chamwino kuna maghorofa yako apartment 100, tatu apartment 60 za vyumba vitatu na apartment 40 vyumba 2 na jengo moja la huduma nalo ni duka," amesema.
"Katika ule mradi wa nyumba 1000 awamu ya kwanza tumejenga nyumba 404 kwa hiyo tunadaiwa nyumba 596 tuweze kumaliza shabaha yetu ya nyumba 1000 Dodoma.




"Huu mradi wa nyumba 300 upande ule au mradi ule wa nyuma kabla ya huu huwa tulikuwa shirika linagharamia gharama za kuleta umeme na maji toka Hayati Magufuli alipotoa lile agizo kule Mtwara kwenye mradi wetu wa Raha Leo wakati anafungua pale aliagiza kwamba watoa huduma watuletee huduma za umeme na maji,"amesema.


"Hilo Mwenyekiti lilifanyika kwenye ile Awamu ya kwanza sisi tulilipia tu gharama za kuunganisha mita hivyo hizo nguzo zote na transfoma,"amesema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments