MWALIKO WA KUHUDHURIA WARSHA YA NAFASI YA VYOMBO VYA HABARI KWENYE KURIPOTI MATUKIO YA KIHALIFU TANZANIA

Chama cha Waandishi wa Habari  wa kupiga vita matumizi ya dawa za kulevya na uhalifu Tanzania (OJADACT) kwa kushirikiana na THRDC  na Jeshi la Polisi Nchini kimeandaa warsha kwa njia ya mtandao ya kujadili nafasi ya vyombo vya habari kwenye kuripoti matukio ya kihalifu. 

Hivi karibuni kumekuwa na matukio ya makundi ya kihalifu kuvamia mitaa na  kujeruhi watu, vyombo vya habari vimekuwa mstari wa mbele kwenye kuripoti matukio hayo, lakini pia kumekuwa na mapungufu wakati wa kuripoti matukio hayo kiasi cha kupoteza mantiki na dhana ya kuelimisha jamii kuachana na uhalifu.

Hivyo OJADACT kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na THRDC tumeandaa warsha hiyo ili tupitishane kwenye njia sahihi ya kuripoti matukio ya kihalifu na kusaidia kutoa elimu kwa  jamii kutojihusisha na matukio yanayohusisha panya road.

Warsha hiyo itafanyika kesho Jumamosi Mei 14, 2022  kuanzia saa 9.00 Alasiri kwa njia ya mtandao wa zoom.

 Mgeni Rasmi
IGP Simon  Siro 

 Wazungumzaji
 1.SACP. David Misime 
Msemaji wa Jeshi la Polisi

 2.Edwin Soko
Mwenyekiti OJADACT

 3.Onesmo Olengurumwa
Mratibu THRDC

 4.Christina Richard 
Kaimu Mkuu Kitengo cha Mwasiliano Wizara ya Mambo ya Ndani

 Link ya mkutano 

Join Zoom Meeting
https://us02web.zoom.us/j/81373269711

Meeting ID: 813 7326 9711
Passcode: 570276

 Muda. Saa 9 Alasiri 
Mei 14.2022

 Kuzuia uhalifu ni wajibu wangu, wako na wetu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments