FISI WATINGA KITUO CHA POLISI SIMIYU...WAKUTWA NA SHANGA NA VYUNGU


Fisi
**
Mkuu wa wilaya ya Bariadi Lupakisyo Andrea, amesema kwamba katika oparesheni ya kuwaangamiza Fisi wilayani humo, wengine wamekuwa wakiwakuta na shanga, huku mapango wanayokaa Fisi hao wakikuta kuna mafiga, vyungu na nyama ambazo zimemalizika kuliwa.

Hayo ameyabainisha mbele ya Kaimu Kamishna wa Uhifadhi wa Idara ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA), Mabula Misungwi Nyanda, aliyefika mkoani Simiyu kwa ziara ya kikazi, ambapo amepata wasaa wa kutembelea familia na kuwafariji watoto walioshambuliwa na kuumizwa na fisi hivi karibuni.


"Kwa hiyo ni kweli wana shanga (Fisi), ukiingia mule ndani kwenya mapango yao utakuta mawe, chungu na nyama ambazo zimetoka kuliwa wakati huo, Mkuu tutaomba utuvumilie, tutajitahidi sana kufuata utaratibu lakini kama wana madhara kwa ulivyojionea, hawa tutaomba tuwaue, tukiweka mtego wa Mbuzi hawali, wanataka mtego wa mtoto ndiyo amle," amesema DC Andrea


"Kinachonishangaza Fisi hawa hawali Mbuzi, pamoja na mitengo ya kisasa ambayo tulikuwa tumeiweka, lakini sasa walikuwa wanashambulia watoto, wawe Fisi wa binadamu au wa Mwenyezi Mungu tuliamua kuingia kupambana nao, ili watoto wasome", amesema DC


Aidha akizungumzia kitendo cha Fisi hao kufika katika kituo cha polisi DC Andrea amesema, "Na kitu ambacho labda kiliwaudhi tuliua Fisi wa mwisho alikuwa na watoto, yaani Fisi anakwenda kituo cha polisi anajua kuna silaha hawa ndio wanatulinda, walipowaona Polisi na silaha zao wao wakaondoka,".


Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments