WAUGUZI WA MANISPAA YA BUKOBA WATAKIWA KUENDELEA KUSIMAMIA MISINGI NA MAADILI YA TAALUMA YAO


Baadhi ya wauguzi wa kituo cha Afya Zamzam wakiapa
Wauguzi wakiwa kwenye maandamano ya maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
Muuguzi Mkuu Kagera ambaye pia ni msimamizi wa shughuli za huduma na ukunga Kagera Mercy Obadia Kagaruki akizungumza kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Mustafa Waziri akizungumza  kwenye maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani
Picha ya pamoja Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Dkt. Mustafa Waziri akiwa pamoja na baadhi ya wauguzi wa kituo cha Afya Zamzam
**

Na Mbuke Shilagi Kagera.

Mganga Mkuu wa Manispaa ya Bukoba Mkoani Kagera Dkt. Mustafa Waziri amewataka wauguzi kuendelea kusimamia misingi na maadili ya taaluma yao ili kujiepusha na kusimamishwa kazi au kufukuzwa.

Ameyasema hayo wakati akizungumza na vyombo vya habari  katika maadhimisho ya siku ya wauguzi Duniani Mei 12, 2022 ambayo katika Manispaa ya Bukoba imefanyika katika kituo cha Afya Zamzam ambapo wamefanya maadhimisho hayo kwa kutembelea wagojwa walio lazwa katika hospitali ya binafsi E.L.C.T Kisha kuandamana mpaka Kituo cha Afya Zamzam.

Katika maadhimisho hayo wauguzi wamefanya kiapo ambacho huwa ni taratbu ya kawaida katika siku kama hiyo ya wauguzi Duniani na kwamba kiapo hicho kinawakumbusha ni namna gani wanatakiwa kutekeleza majukumu yao kwa kufanya kazi kwa weledi na kutotoa siri za wagojwa.

Dkt. Mustafa Waziri amesema kuwa Kituo cha Afya Zamzam kimekuwa kikitoa Huduma kwa wananchi wengi wa maeneo tofauti tofauti ndani na nje ya Bukoba na kusifiwa kutoa huduma nzuri kwa wagonjwa na kwamba tangu kituo hicho kimeanza kutoa huduma za upasuaji, tayari wamefanya upasuaji zaidi ya 366 ambayo imekuwa ikinusuru wananchi wengi zaidi.

"Kwa hiyo na mimi niwapongeze wauguzi wangu kwa kazi nzuri wanazofanya katika kuboresha huduma katika kituo cha Zamzam",amesema

Kwa upande wake Muuguzi Mkuu Mkoa wa Kagera Mercy Obadia Kagaruki ambaye pia ni msimamizi wa shughuli za huduma na ukunga Kagera amesema kuwa katika Mkoa wa Kagera wamejipanga kuboresha huduma na kupunguza au kuondoa kabisa vifo vya mama na mtoto na kuwataka wauguzi wenzake kutoa huduma bora wakiwa kazini na kuwajibika kwa wananchi na kuwaona ni wamoja.

Naye Farida Rashidi ambaye ni mama aliye jifungua katika kituo cha Afya Zamzam amewashukuru wauguzi wa kituo hicho kwa kutoa huduma nzuri na bora wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments