WAZIRI DKT CHANA: SUALA LA UTALII NI LETU SOTE - MALUNDE 1 BLOG | Fahari ya Shinyanga

Breaking

Post Top Ad

Thursday, May 19, 2022

WAZIRI DKT CHANA: SUALA LA UTALII NI LETU SOTE


Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana akipata maelezo eneo la Mapokezi akiwa sambamba na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Shogo Mlozi Sedoyeka wakati alipotembelea Chuo cha Taifa cha Utalii- NCT kampasi ya Bustani leo jijini Dar es salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika eneo maalum la mafunzo ya vinywaji wakati alipotembelea Chuo cha Taifa cha Utalii- NCT kampasi ya Bustani leo jijini Dar es salaam Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana akiwa katika eneo maalum la jiko la mafunzo wakati alipotembelea Chuo cha Taifa cha Utalii- NCT kampasi ya Bustani leo jijini Dar es salaam. Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Dkt Pindi Chana wakati akizungumza na Menejiment ya Chuo cha Taifa cha Utalii- NCT kampasi ya Bustani leo jijini Dar es salaam.

..........................

NA MUSSA KHALID

Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt Pindi Chana amesema tangu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuzindulia Filamu ya Royal Tour watalii wameendelea kuongezeka nchini.

Dkt Chana ameeleza hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipofanya ziara ya kutembelea Chuo cha Taifa cha Utalii- NCT kampasi ya Bustani kwa lengo la kuangalia shughuli mbalimbali zinazofanywa Chuoni hapo ambapo amesema Royal Tour inakenda kufungua malengo zaidi katika sekta ya utalii na kuleta ajira kwa vijana.

Waziri huyo wa Maliasili na Utalii amekipongeza Chuo cha NCT kwa kuendelea kuboresha mitaala ya walimu sambamba na kuwafundisha wataalamu wataalamu wa kuweza kuendesha sekta ya utalii kusaidia kuwaongoza watalii wanaoingia nchini.

‘Nitoe wito kwa wadau mbalimbali kwamba suala la utalii ni la watu wote hivyo ni vyema tukaendelea kuutangaza utalii wetu kupitia sekta mbalimbali jambo litakalosaidia kuwapokea wageni wengi nchini’amesema Waziri Dkt Chana

Aidha Waziri Dkt Chana amesema malengo ya Serikali ni kuhakikisha utalii wa Tanzania unaendelea kukua ili mtalii anafika nchini aweze kurudi kwa mara nyingine kutokana na kuvutiwa na vivutio mbalimbali vilivyopo nchini yakiwemo maeneo ya malikale.

Amesema ni vyema wakaendelea kuwa wabunifu kuangalia soko linataka nini kwani kwa sasa kumekuwa na mashindano kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo ni vyema tukahakikisha tunautangaza vyema utalii wetu.

Awali akizungumza Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii Shogo Mlozi Sedoyeka amesema vipaumbele vyao ni kuboresha mafunzo kwa wanafunzi na kuendelea kutengeneza mitaala mpya ili kuweza kuzalisha watoa huduma bora watakaosaidia sekta ya utalii kuendelea kukua nchini.

‘Mhe Waziri Mikakati mbalimbali tuliyonayo ni kuhakikisha tunaanzisha kampuni ya uendeshaji wa Shughuli za chuo ambayo kwa sasa inaitwa ‘Utalii na Ukarimu Limited Company ambayo lengo lake ni kufanya biashara mbalimbali ili kuongeza pato la chuo na hivyo kupunguza utegemezi kwa serikali’amesema Shogo

Hata hivyo Dkt Chana ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa vyuo mbalimbali nchini kuendelea kuziona kozi za utalii kwani utalii ni jambo la kila siku na ni suala la watu wote kwa kuwa linaongeza mapato ya kutosha nchini.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Pages