Breaking

Post Top Ad

Tuesday, May 10, 2022

WADAU WACHAMBUA RASIMU MPANGO KAZI WA HAKI ZA BINADAMU
Wadau wa asasi za kiraia leo Jumanne, tarehe 10 Mei 2022, wamekutana kwa ajili ya kujadili rasimu ya mpango kazi wa pili wa taifa wa haki za binadamu (2021-2026).


Kikao kazi hicho cha kuhakiki rasimu ya mpango wa pili wa haki za binadamu, kimeandaliwa na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) pamoja na Wizara ya Katiba na Sheria na kufanyika jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika kikao kazi hicho, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria, Dk. Khatibu Kazungu, amewataka wadau hao kushiriki kikamilifu katika kutoa maoni yatakayoboresha rasimu hiyo ili ianze kufanya kazi rasmi.

"Ni matarajio yangu kwamba mtaweza wasilisha michango yao juu ya namna ya kuboresha  rasimi ya mpango kazi. Naamini baada ya kupitia rasimu iliyopo mtatoa michango yenu kikamilify kwa kuwa mchakato unaendelea zoezi hili ni muhimu kuhakikisha Serikali inakamilisha wajibu wake wa kukuza na kulinda haki za binadamu," amesema Dk. Kazungu.

Dk. Kazungu amesema rasimu hiyo umezingatia masuala mbalimbali yanayohusu haki za binadamu na watu Tanzania, ikiwemo haki za kiraia na kisiasa, haki za kiuchumi na utamaduni na haki za makundi maalumu.

"Moja ya haki za kiraia na kisiasa, yafuatayo  yamezingatiwa ikiwemo upatikanaji wa haki na usawa mbele ya sheria, uhuru wa mawazo na kujieleza na kuoata taarifa. Kwenye haki za kiuchumi, utamaduni na kijamii, imezingatua haki ya kuoata maendeleo na kuishi kwenye mazingira safi na salama," amesema Dk. Kazungu.

Naye  Mratibu wa THRDC, Onesmo Olengurumwa, amesema asasi za kiraia zitaendelea kutoa ushirikiano wake kwa Serikali, katika umiarishaji haki za binadamu.

"Mchakato huu unazingatia hatua tano,hatua ya kuoata maoni na uandaaji, ufuatiliaji, utekelezaji na hatua ya kufanya tathimini na yote hii asasi tumekuwa wadau wanaosimamia utekelezaji haki hizo. Asasi tupo pamoja  na Serikali yetu na tutaendleea kuendeleza ushirkiano," amesema Olengurumwa.

Kwa upande wake wadau walioshiriki kikao kazi hicho, wameipongeza Serikali kwa kutambua mchango wa asasi za kiraia katika uimarishaji haki za binadamu nchini.

Evaline Lyimo, kutoka Shirika la Save Mother and Children of Central Tanzania, amesema “ni matarajio yetu katika mpango huu utatusaidia kushirikiana na Serikali, hasa mkoa wangu wa Singida tutaweza kusukuma kazi zetu kwa ushirikiano mkubwa na Serikali.”

Naye Samuel Nsokolo, kutoka Shirika la Development Agency, amesema Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, imeonesha nia ya kushirikiana kwa karibu na asasi za kiraia, tofauti na miaka kadhaa iliyopita.

“Matarajio yetu baada ya kikao kazi hiki, tunafikiria itakuwa tumeimarisha mashirikiano kati ya Serikali na asasi za kiraia, ambapo kwa kipindi cha nyuma karibu miaka mitano tumeona kuna tatizo la mashirikiano na kufanya asasi kushindwa kutekeleza majukumu yake,” amesema Nsokolo.

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Pages