
Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wadau mbalimbali wa vyombo vya habari kutoka ndani na nje ya Tanzania Leo Jumapili Mei 1, 2022 wamefanya Mkutano wa kwanza kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ambayo itafanyika Mei 3 Jijini Arusha. Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa mikutano Hoteli ya Gran Melia ukiongozwa na Kauli mbiu ya mwaka huu ni 'Uandishi wa habari na changamoto za kidigiti'.
Miongoni mwa wadau waliopata nafasi ya kuzungumza katika mkutano huo ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Bi. Salome Kitomari ambaye amesema vyombo vya habari vinaposherehekea siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani bado waandishi wa habari wanakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kutokuthaminiwa kwa waandishi wa habari, kuwepo kwa sheria nyingi zinazombana Mwandishi wa habari pamoja na kuwa na hali duni ya kiuchumi kwa waandishi wa habari jambo ambalo linapaswa kutafutiwa mwarobaini ili kutatua changamoto hizo.


Wadau wa habari wakiwa katika mkutano wa Uhuru wa Vyombo vya habari uliofanyika Jijini Arusha. Kushoto ni Mkuregenzi wa TBC, Ayub Rioba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika (MISA) tawi la Tanzania (MISA-TAN) Bi. Salome Kitomari na Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Kajubi Mukajanga.
Mwenyekiti wa MISA TAN, Salome Kitomari akizungumza katika siku ya kwanza kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani uliofanyika Jijini Arusha

Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Mello akielezea kuhusu Usalama wa Data na Faragha wakati katika siku ya kwanza kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani uliofanyika leo Mei 1, 2022 jijini Arusha
Mkurugenzi wa JamiiForums, Maxence Mello akielezea kuhusu Usalama wa Data na Faragha wakati katika siku ya kwanza kuelekea Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani uliofanyika leo Mei 1, 2022 jijini Arusha


Wadau wa habari wakiwa katika mkutano wa Uhuru wa Vyombo vya habari uliofanyika Jijini Arusha
Social Plugin