Breaking

Post Top Ad

Saturday, May 7, 2022

ZUCHU AILAUMU TCRA, BASATA KUFUNGIA VIDEO YAKE NA DIAMOND PLATNUMZ 'MTASUBIRI '


Kaimu Katibu Mtendaji BASATA Matiko Mniko kushoto, kulia ni Diamond Platnumz na Zuchu

***

Wakati Kaimu Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) Matiko Mniko akimshauri Diamond Platnumz na Zuchu kufanya marekebisho ya video yao ya Mtasubiri ambayo imefungiwa na TCRA na BASATA.

Matiko Mniko anasema video yao itaruhusiwa na kuendelea kuruka hewani endapo wakifanya marekebisho.

Hata hivyo kutoka Lebo ya WCB msanii Zuchu amewajibu Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kuwaambia wamewaonea kuifungia video ya mtasubiri aliyofanya na Diamond Platnumz.

Zuchu ameeleza hilo kwa kutuma ujumbe kupitia Instagram yake kwa kuandika

HII HAPA BARUA YA ZUCHU KWENDA TCRA na BASATA

Ni matumanini yangu mpaka sasa kila mtu anafahamu kua Video Ya wimbo wetu pendwa “MTASUBIRI “ Umesitishwa kuonekana kwenye vyombo vya habari Nchini kwetu .Nimeona bora nianze moja kwa moja kwenye mada husika .Jana Nilipokea taarifa hizi kupitia mitandao kama Nyinyi tu mashabiki zetu kwamba wimbo wetu unapigwa marufuku sababu tajwa kua inaleta ukakasi kwenye jamii husika mwisho wa kununukuu .


Awali ya yote niseme kama msanii nilietumia ubunifu kukaa chini na muongozaji wa video yetu takribani siku 4 kuunda stori ambayo kwa utashi wangu na heshima niliyonayo kwa dini zote na madhehebu yake sikuona huu ukakasi unaoongelewa hapa.Nafahamu si kila kazi ya kisanaa itamfurahisha kila mtu lakini kuvunjia heshima dini si kitu ambacho kipo ndani ya weledi wa kazi yetu sababu tunafahamu fika tunao mashabiki wa dini zote na kulinda hisia zao ni moja ya nguzo kuu Kwenye mziki hatueki matabaka .Ifahamike kwamba mimi ndie nilishoot hiyo scene ikinitaka kuwepo kanisani nikiwa nafanya mazoezi ya kwaya sio misa ni mazoezi ya kikwaya nikiwa nimevalia joho lenye stara .Kanisa hili lipo kisarawe na kabla ya kushoot masister walitukagua na kusikiliza kwa makini stori yetu na kuridhishwa nayo ndipo hapo tukapewa ruhusa ya kushoot .Naomba nielekeze malalamiko yangu kwa mamlaka husika BASATA walezi na wazazi nimeambatanisha video na movie baadhi ambazo zimetoka kabla ya mtasubiri vipi hizi hazina ukakasi
.Lakini ni jamii ipi hiyo iliyoleta malalamiko mpaka nyie kufungia video iliyogharimu muda wa siku nne na pesa nyingi kuishoot tena mkaifungia bila hata kutaka kusikiliza utetezi .
Mtasubiri video ni ya kawaida sana A very innocent sweet story .Naumia sababu hii inaenda kudumaza sio tu mziki ila Tasnia nzima kwa ujumla .


INAENDELEAA

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553

1 comment:

  1. Mwambie akaigize na.msikitin kule Kwan hawajifunzi kupiga dufu? Lazima kanisani tu, HATUTAKI

    ReplyDelete

Post Top Ad

Pages