RAIS SAMIA AMUAPISHA MWALIMU WAKE WA HESABU NA KIINGEREZARais Samia akiwa na Mwalimu wake Khadija Mbaraka
**

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, leo amemuapisha Mwalimu aliyewahi kumfundisha masomo ya Kiingereza na Hesabu akiwa kidato cha pili na cha tatu kuwa Kamishna wa Tume wa Utumishi wa Umma.

Akizungumza leo Mei 21, 2022, mara baada ya kumuapisha, Rais Samia amesema kwamba ilikuwa ni ngumu sana kwa upande wake kumuapisha Mwalimu wake huyo.

"Leo nimepata kazi kidogo kumuapisha Mwalimu wangu Bi Khadija, huyu bibi vyovyote alivyo mfupi, mdogo ni mwalimu wangu wa Hesabu na Kiingereza Form Two na Form Three," amesema Rais Samia

Aidha Rais Samia ameongeza kuwa, "Wale wa umri kama kina Bi Khadija, wakokoteni hivyo hivyo twende nao lakini ninajua akili iko vizuri, mimi kanifundisha akiwa kijana mdogo na nilikuwa nathubutu kusimama na kumuiga darasani nikijua anaingia basi nakwenda kwenye blackboard na-act exactly alivyokuwa akifanya na pengine labda ndiyo maana nimekuwa hivi,".

Chanzo - EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments