NSSF MWANZA YAIPONGENZA MPC KWA KUWAKUTANISHA WADAU WA HABARI

Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa


Na Tony Alphonce  -Mwanza 

Meneja wa NSSF Mkoa wa Mwanza Emmanuel Kahensa amezitaka Taasisi mbalimbali zilizopo Kanda ya Ziwa kujitokeza kushiriki katika Usiku wa Waandishi wa Habari na wadau wa  Habari  Kanda ya Ziwa ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi wa Habari  Mkoa wa Mwanza (MPC).

Akizungumza na Waandishi Wa Habari ofisini kwake leo tarehe 30/05/2022,Kahensa amesema usiku huo wa kuwakutanisha wadau wa Habari ni mzuri kwa kuwa inatoa nafasi kwa Taasisi au shirika kuzungumzia kazi wanazofanya mbele ya Vyombo mbalimbali vya habari na matokeo yake habari hiyo huenda mbali zaidi.


"Binafsi niwapongeze sana Mwanza MPC  kwa kuwa mmekuwa mkisaidia kufikisha elimu kwa wanachama wetu wengi kupitia huu Usiku wa Waandishi Wa Habari na Wadau",alisema Kahensa

Akizungumzia  huduma mbalimbali  wanazozitoa,Kahensa amesema  kuwa, wanachama wa NSSF wamekuwa wakinufaika na mafao 7 likiwemo Fao la Uzazi,Fao la Kifo,Fao la Kutokuwa na Ajira,mafao ambayo yamekuwa msaada mkubwa kwa wanachama.

Usiku wa Waandishi na Wadau Wa Habari Kanda ya Ziwa unatarajiwa kufanyika tarehe 03/06/2022 katika ukumbi wa Rock City Mall ambapo hadi sasa wadau mbalimbali wamethibitisha kushiriki usiku huo.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments