BENKI YA CRDB YAZINDUA HUDUMA YA 'MZIGO FLEXI' JIJINI MWANZA


Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kulia) akikata keki kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
**
Benki ya CRDB imezindua rasmi huduma mpya ya ‘Mzigo Flexi’ katika Jiji la Mwanza ambapo kupitia huduma hiyo, wateja katika makundi mbalimbali wakiwemo wajasiriamali na wafanyabiashara watanufaika na riba ya asilimia tisa baada ya kuweka fedha zao katika benki hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo uliofanyika Ijumaa Mei 20, 2022 katika Benki ya CRDB Tawi la Rock City, Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa Emmanuel Ndeonesia amesema benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kubuni huduma ambazo zinamsadia mteja kutatua changamoto zake.

“Safari hii tumekuja na kampeni ya Mzigo Mflexi ambayo itamsaidia mteja kuwekeza fedha zake benki kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitatu na kumwezesha kupata riba ya asilimia tisa ambapo atapata uhuru wa kuchukua faida yake ndani ya mwezi mmoja, miezi mitatu, miezi sita au ndani ya mwaka mmoja kwa hiyo ni huduma ambayo inampa mteja wepesi na uhuru wa kuchagua” amesema Ndeonesia.

Naye Meneja wa benki ya CRDB Tawi la Rock City, Jesca Kikoita amesema huduma hiyo inagusa makundi yote ya wateja wakiwemo wafanyabiashara ama taasisi wanaohitaji kuwekeza fedha zao kwa malengo ya muda mfupi na muda mrefu na wakasubiria kupata faida ya riba ya asilimia tisa itakayowawezesha kutimiza malengo.

Nao baadhi ya wateja wa benki ya CRDB akiwemo Derick Cyriacus pamoja na Amina Kibuga wamesema huduma ya Mzigo Flexi itawawezesha kuwekeza fedha zao na faida itakayopatikana ikawasaidia kuendesha shughuli zao hususani wakati wa dharura ambapo wameipongeza benki ya CRDB kwa kubuni huduma hiyo.

Awali akizundua huduma hiyo, Mkuu wa Wilaya Misungwi Veronica Kessy amewahimiza wananchi wakiwemo wajasiriamali kuchangamkia huduma zinazotolewa na benki ya CRDB ikiwemo Mzigo Flexi ambayo mbali na kupata faida ya riba ya asilimia tisa, pia watanufaika na mikopo yenye riba nafuu itakayowasaidia kujiimarisha kiuchumi huku akitoa rai kwa benki ya CRDB kuendelea kutoa elimu kwa wananchi ili kufahamu na kuchangamkia fursa ya huduma za kifedha.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy akizungumza kwenye uzinduzi wa huduma ya 'Mzigo Flexi' jijini Mwanza uliofanyika katika tawi la CRDB Rock City Mall.
Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Meneja wa CRDB Tawi la Rock City, Jesca Kikoito akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy akizindua rasmi huduma ya Mzigo Flexi jijini Mwanza kwenye hafla fupi iliyofanyika katika tawi la CRDB Rock City.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kulia) pamoja na Kaimu Meneja CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia (kushoto) wakifurahia jambo wakati wa uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi inayowawezesha wateja kuweka fedha zao benki na kujipatia faida ya asilimia tisa.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kulia) akikata keki kwenye hafla ya uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi iliyofanyika katika tawi la CRDB Rock City jijini Mwanza. Kushoto ni Kaimu Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia.
Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito (kulia) akiandaa keki kwa ajili ya kuwalisha wateja na wafanyakazi wa benki hiyo wakati wa uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kulia) akimlisha keki Kaimu Meneja wa benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia (kushoto).
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto) akimlisha keki Meneja wa CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito (kulia).
Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia (kushoto) akimlisha keki Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (katikati). Kulia ni Meneja CRDB tawi la Rock City, Jesca Kikoito.
Kaimu Meneja wa CRDB Kanda ya Ziwa, Emmanuel Ndeonesia (kushoto) akimlisha keki Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (katikati). 
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto) akiwalisha keki wateja wa CRDB kwenye uzinduzi huo wa huduma ya Mzigo Flexi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto) akimlisha keki mfanyakazi wa CRDB wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kulia) akiwalisha keki mfanyakazi wa CRDB.
Wafanyakazi wa CRDB jijini Mwanza wakilishwa keki na Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto).
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto) akiwalisha keki wafanyakazi wa CRDB jijini Mwanza.
Wafanyakazi wa CRDB jijini Mwanza wakilishwa keki na Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (kushoto).
Wafanyakazi na wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
Wafanyakazi na wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
Wafanyakazi na wateja wa benki ya CRDB jijini Mwanza wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
Wafanyakazi benki ya CRDB jijini Mwanza wakifuatilia uzinduzi wa huduma ya Mzigo Flexi.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CRDB jijini Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments