RAIS WA ZIMBABWE AZINDUA SHAMBA KUBWA LA BANGIRais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa

EMMERSON Mnangagwa; ni Rais wa Zimbabwe ambaye amezindua shamba kubwa la bangi kwa ajili ya dawa lenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 27.


Shamba hilo limewekewa kiwanda cha kisasa cha usindikaji ambacho bangi yake itatumika kama suluhisho la matibabu ya kibaiologia na bidhaa za dawa katika soko la ndani na la kimataifa ambapo mradi huo ni kwa ushirikiano na Serikali ya Uswisi kupitia Kiwanda cha Swiss Bioceuticals na Serikali ya Zimbabwe.


Mnangagwa amesema anaipongeza Serikali ya Uswisi kwa kuwekeza ndani ya nchi ya Zimbabwe

Rais Mnangagwa amesema kuwa, ushirikiano huo unaonesha imani ya Uswisi katika kuwekeza ndani ya uchumi wa Zimbabwe huku akisema kuwa Taifa hilo la Ulaya tayari limeshirikiana na Zimbabwe katika miradi mingine kama vile viwanda, usindikaji wa chakula na ujenzi wa taasisi.

Cc; @sifaelpaul

Download/Pakua App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments