YANGA YAICHAPA GEITA GOLD 7-6 KWA MIKWAJU YA PENATI NA KUTINGA NUSU FAINALI ASFC


***************

Na Alex Sonna

YANGA wametinga Nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Azam Sport Federation (ASFC) baada ya kuitoa Geita Gold kwa mabao 7-6 mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.

Geita walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 86 likifungwa na Offen Chikola na Shaban Djuma aliisawazishia Yanga dakika ya 90 kwa Mkwaju wa Penalti baada ya beki wa Geita kuunawa Mpira.

Mpaka dakika 90 zinamalizika timu hizo zilitoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 na ikapelekea kwenda kwenye Mkwaju wa Penalti.

Kwa Matokeo Yanga wametinga Nusu Fainali na watakutana mshindi kati ya Simba au Pamba kutoka jijini Mwanza mchezo utakaopigwa kati ya Arusha au Mwanza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post