UONGOZI WA CHAMA CHA USHIRIKA MACHINJIO YA VINGUNGUTI WALALAMIKIWA KUTOTOA TAARIFA YA FEDHA KWA ZAIDI YA MIAKA 5



Wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti wakiwa katika shuguli zao za uuzaji wa nyama katika machinjio ya Vingunguti Jijini Dar es Salaam
Wafanyabiashara wa nyama katika machinjio ya Vingunguti wakifuatilia mahojiano ya wenzao (hawamo pichani) waliokuwa wakihojiwa na wana habari machinjioni hapo.

January Jonas Mfanyabiashara katika machinjio ya Vingunguti Dar es Salaam akitoa malalamiko yake mbele ya waandishiwa habari juu ya uongozi wao wa ushirika kushindwa kuitisha mkutano mkuu na kusoma taarifa ya mapato na matumizi kwa kipindi cha miaka saba mfululizo toka viongozi hao wachaguliwe kuongoza ushirika huo.
Fredrick Daudi mfanyabiashara Vingunguti
Fredrick Ndahani mfanyabiashara machinjio ya Vingunguti.
Mfanyabiashara ndani ya machinjio ya Vingunguti Shadrack Mabumo akizungumza kuulalamikia uongozi wao kushindwa kuwasomea taarifa ya fedha ya mapato na matumizi wakiwa madarakani.
Mwenyekiti wa umoja wa ushirika wa wafanyabiashara Joel Meshack akizungumza katika Ofisi za Ushirika huo akijibu Malalamiko ya wafanyabiashara hao alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kutolea ufafanuzi tuhuma za wafanyabiashara hao

PICHA ZOTE NA: HUGHES DUGILO

DAR ES SALAAM.

WANYABIASHARA wa Nyama Machinjio ya Vingunguti wameulalamikia uongozi wao kushindwa kuitisha mkutano na kusoma mapato na matumizi tangu walivyoshika nafasi za uongozi kwa zaidi ya miaka mitano sasa.

Wamesema kuwa katiba yao inawataka kila baada ya miaka mitatu lazima wafanye uchaguzi wa viongozi ikiwa sambamba na kuitisha mkutano wa kawaida wa kusoma mapato na matumizi kwa wanachama.

Akizungumzia malalamiko hayo leo kwenye mkutano uliowakutanisha wanahabari kwaniaba wenzake January Jonas amesema wamechoshwa na hali hiyo huku wakiziomba mamlaka zinazohusika kuchukua hatua stahiki dhidi ya viongozi hao ambao wamekaa madaraka kwa zaidi ya miaka saba sasa pasipokuitisha mkutano wowote.


"Ndugu waandishi wa habari sisi kama wanachama kuna kiingilio pindi tuapoingia kwenye ushirika wetu ambapo kila mwanachama anatoa shilingi 60000 .lakini viongozi hawajawahi kusoma mapato na matumizi jambo ambalo linakidhana na katiba yetu",amesema January.


Amesema licha ya changamoto hiyo ya uchaguzi na taarifa za mapato na matumizi lakini pia kuna changamoto zingine mbalimbali zikiwemo za ngozi na damu ambapo wao kama wafanyabiashara wanaona hawatendewi haki sokoni.


Akijibu Malalamiko hayo Mwenyekiti wa umoja wa ushirika wa wafanyabiashara Joel Meshack amekiri kuwepo kwa ucheleweshaji wa kufanyika kwa mkutano nakudai kwamba hiyo imetokana na kachelewa kuijenga ofisi yenyewe.


Pia amesema kuwa kutokana na hapo awali kuwepo kwa changamoto lukuki lakini hivi sasa wamejipanga vyema nakuwahamikishia wanachama wao kuwa mnamo April 27 mwaka huu watafanya mkutano na baadaye watatangaza tarehe ya mkutano mkuu.


Amewataka wafanya biashara kuwa watulivu wakati viongozi wao wanapopanga kukamilisha kwa michakato mbalimbali ambayo wanayo kwa manufaa ya wanachama wao hao ikiwa pamoja na kuitisha mkutano. na kuelekea kwenye uchaguzi Mkuu.


"Niwahakikishie wafanyabiashara kwamba kila kitu kipo sawa na sisi Kama viongozi tupo hatua za mwisho kufanya mkutano na mambo mengine. Na kuhusu wao kama viongozi ni binadamu kama kuna mapungufu mengine ni ya kibadamu lakini kwa ujumla tuna mambo mazuri kwa ajili ya watu wetu."amesisitiza January


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments