AMUUA MTOTO WA MDOGO WAKE, AMUWEKA KWENYE NDOO KISHA KUMTUPA

 Screenshot_20220412-204124_Gallery

Jeshi Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamshikilia Mwanamke aitwaye Latifa Bakari (33) mkazi wa Mabibo jijini Dar es salaam kwa tuhuma za mauaji ya mtoto wa mdogo wake mwenye umri wa miaka miwili (2) na miezi minne.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam ACP Muliro Jumanne Muliro amesema kuwa mnamo Aprili 05, 2022 mtuhumiwa huyo aliachiwa mtoto huyo na mdogo wake kwa lengo la malezi ambapo alitekeleza mauaji hayo baada ya kumpiga kupita kiasi.

"Baada ya kubaini kuwa mtoto huyo amefariki kwa kipigo mnamo April 06, 2022 aliuchukua mwili wa mtoto (marehemu), akaukunja na kuuweka kwenye ndoo ya plastiki kisha kuudumbukiza kwenye kiroba na kwenda kuutupa eneo la River Side Ubungo",ameeleza Kamanda Muliro.

"Baada ya majirani kutomuona mtoto huyo kama ambavyo si kawaida walitoa taarifa Polisi, ambapo Polisi ilimhoji kwa kina mtuhumiwa huyo na akakiri kufanya mauaji hayo na kwenda kuwaonesha Polisi mwili wa mtoto huyo ulipokuwa",ameongeza.

Amesema  mwili wa mtoto umepelekwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na mtuhumiwa atafikishwa Mahakamani haraka iwezekanavyo baada ya mifumo ya kisheria kukamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post