MAPACHA WATATU WANAOFANANA KAMA SHILINGI WATANGAZA KUOLEWA NA MWANAUME MMOJA


Dada watatu pacha wanaofanana kama shilingi kwa ya pili nchini Kenya wamefichua kuwa sasa wanachumbiana na mwanaume mmoja baada ya kumpenda katika nyakati tofauti.

Wakizungumza katika mahojiano na Jalas, pacha hao, Cate, Eve na Mary walisema kuwa kuwa katika uhusiano na mpenzi wao haikuwa jambo ngumu kwa vile wao ni dada wa karibu sana na wamekuwa wakigawana kila kitu tangu umri wao mdogo.

Walivyokutana na mpenzi wao

Cate ndiye alikuwa wa kwanza kukutana na mwanaume huyo na kuwafahamisha wenzake ambao pia walimpenda.

 Hata hivyo, Mary alikiri ndiye anampenda sana mwanaume huyo. Watatu hao wanatarajia kuolewa na mwanaume huyo hivi karibuni.

"Nilimwona na kumwambia Mary juu yake kabla ya Eve pia kujua juu yake na kumpenda. Tunapanga kumuoa na yuko tayari kwa hilo pia,” Cate alisema.

 Kulingana na dada hao, mpenzi wao hukutana nao kibinafsi Jumatatu, Jumanne na Jumatano mtawalia kabla ya tarehe ya pamoja ya chakula cha jioni Ijumaa. 

Watatu hao pia wamejikita katika taaluma ya muziki wa injili.

Japo hii inaweza kuwashtua wengi, pacha watatu wanaofanya kila kitu pamoja wanazidi kuonekana kama kawaida katika enzi hii ya sasa. 

Katika familia nyingi zilizo na watoto pacha, mara nyingi wanalelewa wakifanya kila kitu pamoja kutoka kwa umri mdogo hadi mahali ambapo kuchagua kugawana mume haiwi jambo ngumu kwao.

Chanzo - Tuko News

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments