KINANA ANG'ARA , ATAKA KUIMARISHA HAKI NDANI YA CCM ILI HAKI ITENDEKE NJE YA CCM

Abdulrahman Kinana

Na Dotto Kwilasa, Malunde 1 blog- DODOMA

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi  Samia Suluhu Hassan ameongoza kikao Cha Mkutano Mkuu maalum  ambacho kimempitisha Kwa asilimia 100 Abrahaman Kinana kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Bara.

Mkutano huo ambao umehudhuriwa na wajumbe  na viongozi mbalimbali wastaafu wa Chama na Serikali umepitisha mapendekezo ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kuhusu marekebisho ya katiba ya chama hicho ya mwaka 1977 toleo la 2020

Akiongea  kwenye Mkutano huo  uliofanyika Jana Jijini Dodoma Rais Samia amesema ataendelea kutenda haki Kwa Kila mwanachama kuinua zaidi ili maendeleo .
 Akiongea mara baada ya kuchaguliwa leo,Makamu Mwenyekiti was CCM Abdulrahman Kinana alimshukuru Mwenyekiti wa Chama hicho Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutambua mchango wake kwa chama hicho na kutamani kufanya nae kazi.

“Juzi uliniita nikawa najiulia nimeitiwa nini, nikajua ni katika kusalimiana.Rais akaniambia nataka uwe Makamu Mwenyekiti, nikamwambia sina hiari, sina budi kukubali, napenda kukuhakikishia Mwenyekiti nitajitahidi kadri ya uwezo wangu kufikia matarajio yako,niseme sitokuangusha”

Kinana pia amemshukuru Kamati Kuu kwa kupitisha jina lake, pamoja na wajumbe wa Halmashauri kuu kwa kupitisha na kuidhinisha jina lake na kusema wamempa imani kubwa na kwamba amejifunza mengi kutoka kwao.

“Kama Mangula asingeamua kustaafu, basi leo nisingekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi”

Makamu Mwenyekiti huyo amewashukuru Wenyekiti wote kuanzia Baba wa Taifa mpaka sasa Rais Samia Suluhu Hassan na kusema kuwa mengine ni mapungufu yake mwenyewe.

Kadhalika ametumia nafasi hiyo kuahidi kwenda kusimamia Chama kuwa imara Kidemokrasia na kusimamia haki ya kuchaguliwa bila upeleo na haki.
 
"Tukiweza kuimarisha haki ndani ya CCM,tutaweza kuimarisha haki nje ya CCM,"amesema

Kinana ameeleza kuwa Tanzania ni nchi inayosimamaia na kutetea haki hivyo lazima kusimamia haki na kuikataa dhuluma

"Lazima tutambue kuwa CCM sio mali ya Serikali japo mali hizi zinatokana na CCM,lakini pia hatupokei maelekezo kutoka  Serikalini  ila Serikali inaelekezwa na sisi,"amefafanua na kuongeza kuwa ;

"Serikali msithubutu kutunyanganya hiyo haki kila mwana CCM ana wajibu wa kuitétea serikali lajini inapovunja sheria tuna haki ya kuongea,tusiseme kwa kukejeli wala kufoka tuna vikao vya Chama,tutawaelekeza yale yaliyosemwa na ilani ,si sawa mwanachama kwenda hadharani kuisema Serikali yake vibaya,"amesema Kinana

Licha ya hayo amewataka watanzania kuujenge utamaduni wa kuwatembelea wananchi na kuwasikiliza matatazio yao ili waendelee kuwachagua kwa sababu watatambua kuwa wanawajali na kujali shida zao kwa kuzifanyia kazini kwa njia ya kuzitatua.

"Nina hakika nitapata nafasi ya kutembelea kila mkoa kuzungumza na wanachama kwa niaba ya mwenyekiti wetu kama Katika inavyosema,
nakuahid utumishi ukiotukuka sio utukufu wa kujikweza,"amesema

Licha ya hayo amezungumzia masuala yanayokwamisha maendeleo ya nchi na kueleza kuwa kichaka cha ukabila, kichaka cha udini na kichaka cha ubara na visiwani haviendani sawa na chama hicho.

Tunaweza kutofautiana kwa mengine lakini sisi ni wamoja“Lazima wanachama wawe huru kutoa mawazo, hakuna mwenye hakimiliki ya mawazo, lazima tumsikilize kila mwananchi, na wanachama wakimchagua mtu kwani sisi ni nani wa kupinga”anasema

Amesisitiza kusimamia Demokrasia na kusema ni lazima kusimamia haki.

“Nimekuwa nikimsikia Rais akisisitiza mara zote katika kusimamia haki, nilimsikia akisema Vyeti peke yake siyo sifa, Vyeti viende na uadilifu, kukubalika, Nchi hii inajulikana kwa haki ndani na nje ya Nchi”anasema

Awali akimuelezea Kinana kabla ya zoezi la kupiga kura mmoja wa wa makada wa chama hicho na aliyewahi kushika nafasi za juu katika awamu mbalimbali kwenye serikali ya chama cha CCM, Steven Wasira amesema kuwa Kinana anazo sifa za kuwa makamu mwenyekiti wa CCM kutokana na mambo makubwa aliyoyafanya ndani ya serikali na chama kwa ujumla hususani wakati chama hicho kilipopoteza mvuto na kukabiliwa na upinzani mkali kutoka vyama vya siasa mnamo mwaka 2012.

Katika hatua nyingine mwanasiasa mkongwe nchini Agostino Mrema amekuwa kivutio katika mkutano huo na mkewe mara baada ya kutambulishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Shaka Hamdu Shaka.

Mrema hivi karibuni alifunga ndoa na mkewe huyo ambapo mara baada ya kuingia ukumbini  alioneshwa kwenye TV kubwa iliyokuwepo uwanjani na kuibua shangwe Kwa mashabiki wake..

AJENDA ZA MKUTANO

Moja ya ajenda Kuu za mkutano mkuu maalum wa chama Cha Mapinduzi (CCM)   ni pamoja na marekebisho yaliyofanywa wakati wa uongozi wa Hayati John Magufuli aliyewaondoa makatibu wakuu wa mikoa kuingia katika vikao vya Halmashauri kuu kwa kile kilichoelezwa kupunguza gharama.

Aidha ajenda kuu ya mkutano huo maalumu ilikuwa ni kuliidhinisha jina la kada kindakindaki wa chama hicho Abdulham Kinana lililopitishwa na Kamati  kuu ya CCM na hatimaye kupigiwa kura ya ndio na wajumbe wa mkutano mkuu huo maalumu ambao mbali na ajenda hiyo pia mkutano huo ulifanya marekebisho ya vifungu na kanuni katika katiba yake ikiwa ni pamoja na sehemu ya nane ya marekebisho kwenye ibara ya 91 kifungu kidogo cha kwanza mpaka cha tisa kama anavyoelezea Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments