POLISI DAR : UCHUNGUZI WA AWALI UNAONESHA DALILI KWAMBA PADRI FRANCIS KANGWA ANAWEZA KUWA AMEJIUA

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limesema linachunguza kwa kina tukio la kifo cha Padri wa Kanisa Katoriki, Patrick Francis Kangwa (49) aliyekuwa Paroko wa Parokia ya Mbezi Mshikamano iliyopo wilaya ya Ubungo.

Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro.

Tukio hilo lilitokea tarehe 15/04/2022, mwili wake ulikutwa katika Tenki la Maji lililopo Mtaa wa Sokoine Jengo la Ottman jijini Dar es Salaam katika makazi ya mapadiri.

Aidha, taarifa za awali zinadai kuwa huenda padri huyo alijiua mwenyewe lakini hata hivyo jeshi la polisi linaendelea na uchunguzi zaidi ili kubaini chanzo halisi ya tukio hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post