BENKI YA CRDB YASHIRIKI KONGAMANO LA KUWAJENGEA UWEZO WANAFUNZI WA VYUO VIKUU


Meneja Mafunzo wa Benki ya CRDB, Agnes Robert akitoa Mada kwa wanafunzi wa umoja wa vyuo vikuu AIESEC katika kongamano lililofanyika katika ukumbi wa Nkrumah wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam jana.
Meneja wa Mafunzo na Maendeleo ya Wafanyakzi wa Benki ya CRDB, Edith Myombela akizungumza na Baadhi ya wanafunzi wa Chuo kikuu cha Dar es salaam waliofika kwenye banda lao ili kufungua akaunti.
Benki ya CRDB imeshiriki katika kongamano la umoja wa Taasisi za Elimu ya Juu ya vyuo vikuu vyenye lengo la kuwajengea vijana sifa za uongozi kupitia mafunzo yanayotolewa na Taasisi mbalimbali ambao ni washirika wa umoja huo, ili waweze kuingia katika ushindani na kuzikabili changamoto katika soko la ajira.


Benki ya CRDB imekuwa ni moja ya benki kiongozi nchini katika kuhakikisha inashiriki kuelimisha makundi ya vijana wa vyuo mbalimbali nchini kupitia program mbalimbali yakiwemo Mafunzo kwa vitendo ‘Field attachmets’, Mafunzo kazini '├Źnternship’ na Programu maalumu ya Maendeleo ya wahitimu ‘Apprenticeship’ ambayo yalianzishwa mwaka 2020 kwa kuwachukua wahitimu 29 kutoka nchini Tanzania na 2 kutoka nchini Burundi.


Pia Benki ya CRDB kila mwaka huchukua kati ya wanafunzi 300 hadi 500 na kuwaunganisha katika vitengo mbalimbali vilivyopo ndani ya benki hiyo na kwenye matawi yake yaliyosambaa kote nchini ilikuweza kuwapatia mafunzo ya vitendo.


Wanafunzi wa vyuo nchini wamekuwa wakifurahia huduma mbalimbali za kibenki kutoka Benki ya CRDB ikiwa ni pamoja na upatikananji wa mikopo maarufu kama Boom Advance umekuwa ni mkombozi kwa wanafunzi wengi wanaotumia benki ya CRDB kwakujipatia mikopo rahisi hivyo kurahisisha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kifedha. Pia Benki ya CRDB imewatengenezea akaunti maalumu ya wanafunzi wa vyuo ambayo gharama zake za kufungua akaunti hiyo ni shilingi za Kitanzania Elfu Tano tu (5,000). wastani wa mikopo 20,000 inatolewa kila Mwezi kwa wanafunzi mbalimbali nchini, na wastani wa akaunti 50,000 zinafunguliwa kila mwaka na wanafunzi wanaojiunga na vyuo vikuu nchini.


Kwa miaka mitano sasa Benki ya CRDB imekuwa Mshirika wa umoja wa Taasisi za Elimu ya juu za wanafunzi nchini Tanzania ‘AIESEC’.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post