RAIS SAMIA ASHIRIKI DUA YA KUMUOMBEA HAYATI SHEIKH ABEID KARUME


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la Maua katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50. Picha na Ikulu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume, Mkuu wa Majeshi Jenerali Venance Mabeyo, wakiomba Dua mbele ya Kaburi la Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50 tangu kifo chake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Amani Abeid Karume, na Makamu wa Rais Dkt. Philip Isdor Mpango baada ya kukamilika kwa Dua ya kumbukizi ya kutimia miaka 50 tangu kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume iliyofanyika leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiagana na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa baada ya kukamilika kwa Dua ya kumbukizi ya kutimia miaka 50 ya kifo cha Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abeid Amani Karume iliyofanyika leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, akiwa katika Dua ya pamoja na Mama Mariam Mwinyi, Mama Mbonimpaye Mpango na aliyekuwa Mke wa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume katika Kumbukizi ya miaka 50 ya aliyekuwa Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan akiwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi wakielekea katika Kaburi la aliyekuwa Rais wa Kwanza wa Zanzibar Hayati Sheikh Abeid Amani Karume leo tarehe 07 Aprili 2022 Afisi Kuu ya Chama cha Mapinduzi CCM Kisiwandui Zanzibar ikiwa ni kumbukizi ya Miaka 50 tangu kifo chake

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments