SIMBA YANG'ARA UGENINI..YAIDUNGUA COASTAL UNION 2-1
Na Alex Sonna

MABINGWA Watetezi Simba wameng’ara ugenini baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Coastal Union mchezo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Simba walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 39 likifungwa na Bernard Morrison baada ya beki wa Coastal kufanya uzembe ndani ya kumi na nane Morrison kuuwahi Mpira.

Kiungo Mkabaji kutoka Nigeria Victor Akpan aliisawazishia Coastal dakika ya 76 kwa shuti kali lililoenda moja kwa moja na kumuacha Aishi Manula.

Akitokea benchi Mshambuliaji hatari Meddie Kagera alipigilia msumari wa pili dakika ya 90+2 kwa bao safi huku Coastal walipata pigo dakika ya 87 kwa beki wake Patrick Kitenge kuonyesha kadi nyekundu.

Kwa ushindi huo Simba wamefikisha Pointi 40 nafasi ya pili huku Coastal Union wakibaki nafasi ya 12 wakiwa na pointi 21.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post