SHEIKH WA MKOA MWANZA AHAMASISHA UJENZI WA MISIKITI YA KISASA, KIVULINI WAMUUNGA MKONO

Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke ametoa changamoto kwa misikiti mbalimbali mkoani Mwanza kutafakari na kuanza mikakati ya kujenga misiki ya kisasa yenye ramani ya ghoroma kwani baadhi ya misikiti iliyopo hairidhishi.

Sheikh Kabeke ameyasema hayo Jumapili Aprili 24, 2022 wakati akizungumza na Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda uliopo Kisesa wilayani Magu baada ya kusimama ili kukagua maendeleo ya ujenzi huo akiwa njiani kuelekea Magu kwenye kongamano la 'malezi bora, tabia njema na misingi ya ndoa'.


"Wazee wetu walijinyima wakajenga hii Misikiti ya chini, hatuwezi kuibeza lakini lazima tubadilike tutoke huko, tuanze kujenga Misikiti ya kisasa ya ghorofa", amesema Sheikh Kabeke akiwapongeza waumini wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa kwa kuanza ujenzi wa Msikiti wa kisasa.


Pia Sheikh Kabeke ametumia fursa hiyo kusaidia upatikanaji wa barua ya utambulisho wa wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti huo wanaotarajiwa kusafiri kwenda jijini Dar es salaam kwa ajili ya kutafuta ufadhili wa ujenzi huo huku akichangia shilingi laki moja ili kuunga mkono jitihada hizo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti huo, Hassan Khalid amesema ujenzi huo ulianza mapema mwaka huu 2022 ukitarajiwa kugharimu shilingi Bilioni 1.2 hadi kukamilika na hivyo kuwaomba wadau mbalimbali kuchangia.


Naye mdau wa maendeleo kutoka Shirika la KIVULINI, Yassin Ally amemuunga mkono Sheikh Kabeke kwa kuchangia shilingi laki moja na kutumia fursa hiyo kuwahimiza waislamu kuimarisha umoja ili kufanikisha miradi yao akisema, "tunahitaji BAKWATA imara yenye mifumo thabiti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo na si kama ilivyokuwa awali ambapo BAKWATA dhaifu ilikuwa kwa ajili ya manufaa ya wapigaji".

Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (wa tano kushoto) akiwa na viongozi mbalimbali kukagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akipiga simu kwa Katibu wa BAKWATA Mkoa Mwanza kumhimiza kuandika barua ya utambulisho kwa wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda wanaotarajiwa kusafiri kwa ajili ya kutafuta michango kutoka kwa wadau ili kufanikisha ujenzi huo.
Sheikh wa BAKWATA Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (wa tano kushoto) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa kisasa wa Masjid Al-Huda Kisesa ambapo pia aliongoza Dua kwa wajumbe hao.
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally akitoa salamu na nasaha kwa Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa.
Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa wakifuatilia nasaha kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa KIVULINI, Yassin Ally.
Wajumbe wa Kamati ya Ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa wakifuatilia nasaha mbalimbali baada ya Sheikh wa Mkoa Mwanza (hayuko pichani) kutembelea msikitini hapo.
Karibu kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Masjid Al-Huda Kisesa kupitia Benki ya Amana akaunti nambari 00 61 41 72 61 60 00 1 jina Kamati ya Ujenzi Alhuda Kisa au M-Pesa nambari 0763 39 62 94 jina Hassan Khalid Mohamed.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527

0/Post a Comment/Comments