KIJANA WA MIAKA 25 ATANGAZA KUFUNGA NDOA NA BIBI WA MIAKA 85 MWENYE WAJUKUU 20


Kijana akiwa kwenye mahaba mazito na Bibi mpenzi wake
Mwanaume mchanga mwenye umri wa miaka 25, kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) amewashangaza wengi baada ya kufichua mipango yake ya kufunga pingu za maisha na mpenzi wake wa miaka 85.

Wapenzi hao wanalandana sana wazimu na kuzama katika bahari ya mapenzi na sasa wanapanga kufanya harusi hivi karibuni ili kuweka rasmi uhusiano wao.

 Wote wawili wanaazimia kuishi pamoja maisha yao yote licha ya kwamba mpangilio huo haujawafurahisha wengi.

"Hili ni chaguo langu. Hii ni furaha yangu, kama mtu mwingine yeyote ana yake. Kabla ya kuwafurahisha wengine, kwanza, jifurahie mwenyewe na uamue kutozingatia maoni ya mtu mwingine yeyote," Muima aliiambia Afrimax English.

Muima na wenzake walikuwa wakiwinda nyumba walipotua nyumbani kwa Thereza, ambapo walilipa kodi na kuanza maisha mapya.

 "Jinsi alivyotenda na kunijali (mimi) kulinichochea kumpenda na ingawa yeye ni mwanamke mzee na kwa kweli, anaweza kuwa nyanya yangu lakini ninampenda," Muima alisema. 

Alisimulia siku ambayo mwenzake hakuwepo, na alikuwa anakeketwa na njaa na hakuwa na chakula katika nyumba yake ya kupanga. Mwanamke huyo alimletea chakula na kumpa kwa uangalifu sana kabla ya kuomba busu, ambayo alikubali kumpa.

Uhusiano huo ulipozidi kuimarika, wapenzi hao walitumia muda wao kucheza, kuinuana na kusafiri licha ya umri wa Thereza. 

Ananipenda na pia mimi nampenda Watu wengi ambao hawafahamu uhusiano wao hufikiria ni bibi anafurahia wakati wake na mjukuu wake au mwanawe. Thereza ana wajukuu wakubwa kuliko mpenzi wake, lakini haoni aibu kuwa kwenye uhusiano na Muima. "Nina watoto wanane na wajukuu 20. Kulingana na umri wa mpenzi wangu, anaweza kuwa mjukuu wangu wa tano. Ananipenda na mimi nampenda. Niko tayari kuvaa nguo ya harusi na pete," alisema.

Muima yuko tayari kulipa mahari ya ng'ombe 12 ambao watoto wa mpenzi wake wameitisha.

 Mwanaume huyo amepata mapenzi na nyanya huyo baada ya kuwa katika mahusiano mengi ambayo yalikuwa yakivunjika.

 "Sitawahi kuchagua msichana yeyote zaidi ya huyu. Naomba asife kabla yangu," Muima aliongeza. Thereza hakupuzilia uwezekano wa kuanzisha familia na mpenzi wake mchanga, akisema kuna mifano katika Biblia inayompa tumaini.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post