RADI YAUA NA KUJERUHI SHAMBANI

Watu wawili  wamefariki dunia na wengine wawili kujeruhiwa baada ya kupigwa na radi katika kijiji cha Idiwili ,Mbozi mkoani Songwe leo jioni ya Aprili 6, 2022.


Afisa Mtendaji wa Kata  ya Idiwili, Carolina Kikoti amethibitisha kutokea tukio hilo na kueleza kuwa radi hiyo iliwapiga wakiwa shambani.

Amewataja waliofariki dunia kuwa ni Stenala Mwambongoro (54) na mtoto wake Raheli Msongole (16) wakati  majeruhi ni Sephania Mwasenga na Tabia Haonga majeruhi wanaendelea kupatiwa matibabu katika kituo cha Iyula kilichopo Mbozi Songwe.


Chanzo :  https://www.instagram.com/p/CcA2eKUtFzY/?utm_medium=copy_link

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post